Jeshi
la polisi nchini limeondoa marufuku ya mikutano ya ndani kwa vyama vya
siasa kwa madai kwamba limeridhishwa na hali ya kiusalama iliyopo
nchini.
Kamishna
wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani Mssanzya
ametangaza kuondoa zuio hilo leo na kusema kuwa makatazo mengine ya
mikutano ya vyama hivyo yako pale pale.
Mssanzya
amesema mikutano ya hadhara na maandamano bado hairuhusiwi lakini
wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao katika majimbo yao kwa mujibu
wa katiba.
"Maandamano na mikutano ya hadhara imezuiliwa hadi tathmini pana zaidi ya hali ya usalama itakapofanyika," amesema Mssanzya
Post a Comment