Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib wa pili kulia akisoma ramani ya eneo la kukabidhiwa mchezaji bora Afrika, Mbwana Samatta wakati wa kupima eneo hilo atakalokabidhiwa jumapili. Kulia ni mchezaji wa zamani ya Stars na YAnga, Salvatory Edward na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa SHIWATA, Mohamed Kisoky
Na Mwandishi Wetu
Sherehe za kukabidhi kiwanja cha ekari tano kwa mchezaji bora barani Afrika, Mbwana Ali Samatta unafanyika Jumapili 5,2016 kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.
Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Klabu ya Yanga, Salvatory Edward (kulia) akisaidia kupima eneo atakalokabidhiwa mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga
Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Klabu ya Yanga, Salvatory Edward (kulia) akisaidia kupima eneo atakalokabidhiwa mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga
Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha idadi ya wanachama 180 waliokwisha kabidhiwa nyumba zao.
Taalib alisema mtandao huo unaomiliki eneo la ekari 300 za kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji.
Sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185 wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana.
HITACHI
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ambaye atakuwa Waziri wa pili kutembelea kijiji hicho baada ya Naibu Waziri wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka huu.
Viongozi wengine waliowahi kutembelea kijiji hicho ni kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2014, Wakuu wa wilaya ya Mkuranga wastaafu, Mercy Silla, Clemency na Mkuu wa wilaya hiyo wa sasa, Abdallah Kihato.
Wageni wengine walioalikwa kwenye sherehe hizo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi viongozi wa Serikali wa Wilaya ya Mkuranga na wasanii maarufu nchini.
Post a Comment