Sherehe hizi zitafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam tarehe 22/06/2016 ambapo mgeni rasmi atazindua vitabu viwili na kufuatiwa na kongamano litakaloshirikisha wataalam mbalimbali wa uchumi wakiwemo magavana 20 wa benki kuu kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mada kuu katika Kongamano hilo itakuwa: “Beyond Aid and Concessional Borrowing: New Ways of Financing Development in Africa and its Implications”, (yaani namna ya kupata fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya misaada na mikopo nafuu na athari zake) itakayowasilishwa na Prof. Justin Lin wa Chuo Kikuu cha Peiking, China. Mada hii imechaguliwa kwa kuzingatia changamoto ambazo serikali za Afrika zinakumbana nazo katika kugharamia miradi ya maendeleo wakati ambapo misaada na mikopo nafuu imekuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa.
Wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) watashiriki katika kongamano hilo.
Post a Comment