0
                
                     Maafisa wa polisi nchini Tanzania
Polisi hapa nchini wamepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia Jumanne wiki hii hadi hali ya usalama itakapotulia.

Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari walinda usalama hao wamewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.

Taarifa hiyo imesema kuwa polisi hawatasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hilo.

Aidha maafisa hao wamewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa taifa la Tanzania.

Polisi hapa nchini imeripoti kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya kisiasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano .

Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.

Post a Comment

 
Top