Mstaiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni
Boniface Jacob amesema wananchi wote ambao wamewekewa alama za X kwenye
nyumba zao na hawana mlalamiko yoyote ambayo yanafahamika kisheria na
mahakama, wabomoe nyumba zao kwa hiari yao.
‘’Mtu akiwekewa alama ya X anatakiwa
ndani ya siku 14 kama ana malalamiko yoyote aweze kupeleka mahakamani
kwa ajili ya kuweka zuio na hili litafanikiwa kama ana hati ya nyumba na
vielelezo vyote vinavyohitajika kisheria’’-Amesema Mstahiki Meya.
Aidha Meya amesema kwamba kwa nyumba
zote ambazo zipo katika maeneo ya wazi na ambayo yabebainishwa kisheria
kama maeneo ya umma na kuwekewa X nyumba hizo zitabomolewa muda sii
mrefu baada ya kukamilika kwa kijiko cha kubomoa ambacho kilikuwa
kimeharibika.
Hata hivyo Meya amesema watu wote
waliowekewa X maeneo yote ya maskini na matajiri yatabomolewa nyumba zao
hivyo hakuna mtu ambaye atakuwa juu ya sheria.
Kwa upande mwingine Meya amewataka
wananchi ambao wamebomolewa nyumba zao maeneo ya mabondeni na wameanza
kurejea watambue bado serikali ipo na itawaondoa hivyo ni bora watafute
utaratibu mwingine.
Post a Comment