Abiria wa mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es salaam leo June 20
2016 wameanza kutumia kadi maalumu za kielektroniki badala ya
tiketi. Mfumo huu ambao utamuwezesha abiria kuweka fedha katika kadi hio
kwa kutumia mitandao ya simu na utasaidia kupunguza msongamao katika
vituo vya ukataji tiketi.
HAYA NI MAMBO MATANO YA KUFAHAMU
1.Unapokwenda
kununua kadi utapewa maelekezo ya namna ya kujisajili, kuna namba ya
*152*22# ukipiga namba itakupa maelekezo, utachagua kwenye menu
litatokea neno DART itakupa maelekezo kama unajisajili utatakiwa kujaza
namba ya kadi, utajaza majina yako na utaweka namba yako ya siri.
2.Ukipoteza
kadi hatua ya kwanza unaweza kuifunga isitumike na mtu mwingine kwa
kubonyeza *152*22# unachagua DART itakuja option ya kuifunga.
3.Kadi
ikinunuliwa tayari ina muda wa kusafiri, kwamba hutalazimika kufanya
Top up baada ya kuinunua, kadi utainunua 500 lakini utakuwa na muda wa
kusafiri wa sh 4500, baada ya kuwa umeshainunua unaweza kusafiri muda
huohuo.
4.Ukipoteza
kadi na ukitaka kupata mpya, kama iliyopotea ina muda wako wa kusafiri
taarifa zako zitasaidia kupata kadi mpya na utarudisha pia salio lako
ambalo litakuwa limebaki.
5.Wanafunzi
wataendelea kutumia tiketi kwa sababu mfumo wa tiketi pia bado
utatumika sanjari na matumizi ya kadi, usajili wa mwanafunzi ili wapate
kadi zao utachukua muda.
Post a Comment