Mkurugenzi wa Petrol kutoka EWURA injinia Godwin Samweli amekanusha taarifa hizo na kusema hakuna
upungufu wa mafuta ya taa nchini kwa sababu yapo ya kutosha na meli
kubwa imemaliza kushusha lita milioni 2.5 ambazo zitatumika kwa siku 20
na mengine yapo kwenye matanki.
>>>tuna
mafuta mengi tu, mengine yameshuka leo na mengine yako kwenye matanki,
kila mwezi lazima kuna shehena ya mafuta ya taa inakuja, kwa siku moja
kwa matumizi yetu ni kama lita 126,000‘
>>>’hakuna
mfanyabiashara atakuwa na pampu ya mafuta ya taa halafu akatae kuuza
mafuta ya taa, kama kuna mkoa mmoja au miwili ambayo imetokea hivyo
huenda gari limeharibika njiani, lakini wafanyabiashara wako makini sana
kufanya biashara, kama mafuta yapo hapa Dar es salaam ni lazima
watayapeleka kwenye vituoa vyao‘
Post a Comment