0


Mkuu wa wilaya ya Liwale mh.Ephraim Mmbaga, picha hii iliyopigwa na Liwale Blog kwenye mahafali ya kidato cha nne Liwale high school Septemba mwaka 2015

Alikuwa mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,mh.Ephraim Mmbaga baada ya Rais Magufuli kutangaza wakuu wapya wa wilaya june 26 ameweza kufunguka kwenye mtandao wa kijamii wa facebook kwa kuandika ujumbe huu hapa chini.

TANZANIA NCHI YETU SOTE.
Hili ni taia letu sote. Hata nafasi za uongozi uwe wa kuchaguliwa au ule wa kuteuliwa hauwezi kuwa hati miliki ya kundi la watu fulani. Fursa hizo hazina budi kuwa zetu sote kwa kuwa tayari kupokezana vijiti.


Miaka takribani 5 iliyopita nilibahatika kuwa miongoni mwa wateule wa Mhe Rais. Nilipata fursa hiyo huku makada wenzangu wengi wakikosa fursa hiyo.


Zamu hii mamlaka ya uteuzi imeniambia kaa benchi, mchezaji mwingine achukie fursa hiyo mchezo uendelee. Nisipopokea agizo hilo la kocha wangu kwa shukrani na unyenyekevu mkubwa ukomavu wangu kisiasa na kimaadili una kasro kubwa.


Karibu Liwale mpambanaji mahiri Dc Mteule Mhe Sarah Vincent Chiwamba. Kwaherini wananchi wa Liwale na mkoa wa Lindi kwa ujumla. Niwashukuru sana kwa upendo na ushirikianio mlionipatia. Nitawakumbuka muda wote wa maisha yangu. Aidha niombe mniwie radhi wale wote ambao yawezekana niliwakwaza kwa njia moja au nyingine katika muda wote nilikuwa nanyi 9/5/012_ 26/6/2016. Pamoja Daima.


Post a Comment

 
Top