0


Wavuvi wa manispaa ya Lindi wanakumbwa na changamoto nyingi katika shughuli zao za uvuvi baharini.

Kutokana na changamoto ambazo wanazipata baadhi ya wavuvi manispaa ya lindi mjini wameamua kuunda umoja wao ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo lakini pia waweze kujulikana kwa uraisi.

Akizungumza na mwandishi wetu mwenyekiti wa chama hicho cha wavuvi manispaa ya lindi bwana Swalehe Kazumari amesema wavuvi wamekuwa wanakumbwa na changamoto nyingi na zimekua hazitatuliwi kutokana na kutokuwepo na umoja.

Aidha amesema kuwepo kwa chama hicho kitasaidia kujijua wapo wangapi na kama, kutakuwa na tatizo lolote basi watajulikana walipo.

Post a Comment

 
Top