Shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea..
Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa watu hao 32 na idadi hiyo ya majeruhi.
Mashuhuda
wanasema waliwaona washambuliaji watatu,ambapo mmoja kati yao alikuwa
akifyatua risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa bomu na
kufa.
Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja huo.
Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.
Uturuki
imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi kutoka pande
mbili,kwanza kutoka kwa kundi la Islamic State wanaoingia kutoka nchi
jirani ya Syria na waasi wa Kikurud wanataka kuunda dola yao.
Post a Comment