Kushoto ni Meneja wa shirika la Nyumba la taifa mkoa wa Kigoma (NHC) Nistasi Mvungi akikabidhi Madawati 50 kwa mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia jeneral Emanuel Maganga katika shule ya msingi Rubuga.
*****
BENKI ya NMB imekabidhi jumla ya madawati 150 yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa mkuu wa mkoa Kigoma Emanuel Maganga ikiwa ni kuitikia agizo la raisi John Pombe Magufuli ili kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.
Akikabidhi madawati hayo kwa mkuu wa mkoa Kigoma Meneja wa Kanda ya Magharibi wa benki ya NMB,Leon Ngowi amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango wa benki hiyo kutumia kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii hasa ya elimu na afya hapa nchini kwa mwaka huu wa fedha.
Ngowi alisema kuwa misaada hiyo inayotolewa na benki hiyo ni ikiwa sehemu ya michango inayotoka kwa wateja wenye akaunti katika benki hiyo na hiyo ni kurudishe sehemu hiyo ya faida kwa wananchi.
Akipokea msaada huo mkuu wa mkoa Kigoma, Emanuel Maganga ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na kusema kuwa hiyo inaonyesha namna wadau mbalimbali mkoani humo wanavyoguswa na adha wanazopata watoto katika shule.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa amepiga marufuku madawati ya shule za msingi na sekondari mkoani humo kutumika kwa ajili ya sherehe mbalimbali za watu binfasi ndani na nje ya shule, akieleza kuwa kuhamishwa kwa madawati hayo kila wakati kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwani kunachangia kuyafanya kuharibika haraka.
Wakizungumza baada ya kupokea madawati hayo, mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Rubuga,Leonadus Mtonto na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kutolewa kwa madawati hayo kutawaondolea adha ya baadhi ya wanafunzi kukaa chini na kuinua kiwango cha taaluma shuleni hapo.
Wakati huo huo Shirika la nyumba la taifa (NHC) mkoa Kigoma limekabidhi kwa mkuu wa mkoa Kigoma jumla ya madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5 ikiwa kutekeleza ahadi iliyotoa katika harambee ya kukabiliana na madawati mkoani Kigoma iliyoitwa na mkuu wa mkoa huo Emanuel Maganga.
Akikabidhi madawati hayo kwa mkuu wa mkoa Meneja wa NHC mkoa Kigoma,Nistasi Mvungi amesema kutolewa kwa madawati hayo ni kuunga mkono agizo la rais John Magufuli la kukabiliana na upungufu wa madawati nchini.
Akizungumza baada ya kupokea madawati hayo mkuu wa mkoa Kigoma,Emanuel Maganga alisema mkoa huo umetekeleza agizo hilo kwa kuondoa upungufu huo wa madawati mkoani humo.
Na Rhoda Ezekiel-Malunde1 blog Kigoma.
Post a Comment