WATUMISHI hewa 14 wameongezeka katika Halmashauri ya wilaya ya
Kinondoni, hivyo kuongeza idadi ya jumla ya watumishi hewa 103 ambao
wameiingizia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 1.5.
Aidha, kati ya watumishi hao, 16 wameanza kurudisha fedha walizokuwa wakilipwa ambazo ni zaidi ya Sh milioni 9.4 Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi alisema kuwa alipoingia madarakani alikuta watumishi hewa 34 na kuongezeka hadi 89.
‘’Baada ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda kuwalisha kiapo wakuu wa idara, watumishi hao waliongezeka kutoka 34 na kufikia 103,’’ alisema Hapi. Alisema pia wakuu hao wa idara wameongezewa muda wa kuendelea kukusanya taarifa za watumishi hewa waliopo kwenye idara zao.
Katika hatua nyingine, halmashauri hiyo imetenga Sh bilioni tatu kwa ajili ya mkopo kwa vijana na wanawake, watakaojiunga kwenye vikundi vya wajasiriamali ili kupambana na umasikini na kuinua kipato.
Alisema katika ‘Operesheni Safisha Kinondoni’ wamefanikiwa kukamata wazururaji 10 na wapiga debe saba, ambao wameshtakiwa kwa makosa ya kubughudhi abiria katika vituo vya daladala.
‘’Tunatarajia kuwa na programu kubwa ambayo itawashirikisha vijana na wanawake. Tumepanga kuwaita wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara kuja kutoa mafunzo ya namna ya kuwa wajasiriamali ikiwamo kutengeneza uyoga,’’ alisema Hapi.
Alisisitiza kuwa fedha ambazo serikali imepanga kutoa katika mwaka wa fedha wa 2016/17 za Sh milioni 50 kwa kila kijiji, zitawasaidia wanawake na vijana watakaojiunga na vikundi na kujisajili.

Post a Comment