Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV Magogoni umeanza rasmi mara baada ya kusitisha huduma zake hivi karibuni.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea eneo la bandari kujionea kazi ya ukarabati kwa
kivuko hicho, Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole-kujan
amesema kazi ya ukarabati wa kivuko hicho umeanza kwa hatua za awali za
kukifanyia usafi ili kuona maeneo yaliyoharibika na kuyafanyia
ukarabati.
“ Muda
wake wa matengenezo umefika na ni wakati muafaka kwa kivuko kufanyiwa
matengenezo ni muda mrefu kimehudumia wananchi wa Jiji la Dar es Salaam
lakini mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kitarudi kutoa huduma
kama kawaida” Alisema Mhandisi Manase.
Mhandisi
Manase ameongeza kuwa ukarabati huo utazingatia viwango vya kimataifa
ili kukiwezesha kivuko hicho kudumu kwa muda mrefu bila ya kupatwa na
hitilafu yoyote ya kiufundi na kuwaasa wahandisi husika kufanya
ukarabati huo na kukamilika kwa muda uliopangwa.
Aidha
Mhandisi Mkuu Kutoka kampuni ya Songoro Marine Boat yard LTD Major
Songoro amesema kwa kushirikiana na waandisi kutoka TEMESA watahakikisha
wanamaliza kazi ya ukarabati kwa wakati na kwa ufanisi wa hali juu ili
kurejesha huduma ya Kivuko hicho.
Kivuko
cha MV Magogoni kinachotoa huduma eneo la Magogoni na Kigamboni Jijini
Dar es Salaam kimesitisha kutoa huduma kwa ajili ya kufanyiwa
matengenezo makubwa na kwa sasa kivuko cha MV Kigamboni kinashirikiana
na MV. Lami kutoa huduma kwa wananchi.
Post a Comment