Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(Katikati)akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, (hawapo pichani) wakati wa
kutangaza baadhi ya wanamuziki nchini ambao watatoa burudani pamoja na
Mwanamuziki nguli kutoka Marekani NE-YO, katika Uwanja wa (CCM) Kirumba
jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom Festival 2016.Wengine
katika picha kushoto ni Mwakilishi wa NE-YO,E.Jay Mathews na Mkurugenzi
Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt.
Sebastian Ndege.
Mwakilishi
wa Mwanamuzi nguli toka nchini Marekani NE-YO, E.Jay Mathews (kushoto)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
kutangazwa kwa wasanii watakaotoa burudani pamoja na mwanamuziki huyo
katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016, litakalofanyika
katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wapili (kushoto) ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha
hilo,Dkt. Sebastian Ndege, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania, George Sozigwa Mkuu wa masuala ya ulinzi na Usalama wa tamasha
hilo.
Mwanamuziki
wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul”Diamond Platinum’s” akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na jinsi
atakavyoshiriki kutoa burudani na kuimba wimbo wa pamoja na mwanamuzi
NE-YO wa nchini Marekani katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival
2016, litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa
tamasha hilo, Dkt. Sebastian Ndege, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa
Vodacom Tanzania.
Moto wa burudani kuwashwa jijini Mwanza Jumamosi ijayo
NE-YO kushusha bonge la shoo kushirikiana na wasanii nguli wa Bongofleva nchini
Wakiwemo Diamond Platinum’s, NEY wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma Nature,Mr.Blue na wengine kibao.
Pia tiketi kupatikana kupitia huduma ya M-PESA
Moto wa
burudani utawaka katika jiji la Mwanza Jumamosi ya wiki ijayo ambapo
msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva kutoka Marekani NE-YO atakapo
shusha bonge ya shoo kwa kushirikiana na wasanii wa hapa nchini katika
uwanja wa CCM Kirumba kwenye onyesho lililotayarishwa na Jembe Media
chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.
Akiongea
juu ya onyesho hilo la kihistoria katika ukanda wa ziwa Magharibi,Meneja
uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inayo
furaha kudhamini tamasha hili kubwa litakaloleta burudani ya muziki kwa
wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Aliwataja
baadhi ya wanamuziki watakaowasha moto kumsindikiza NE-YO kuwa ni
Diamond,Ney wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma
Nature,Mr.Blue,Stamina,JJ Bendi na wengineo .
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha
hilo, Dkt.Sebastian Ndege aliwataka wapenzi wa muziki kujitokeza kupata
budurani ya mwaka katika tamasha hilo na mipango ya tamasha hilo kubwa
imekamilika na kuwataka wapenzi wa muziki wa Mkoa wa Mwanza wakae mkao
wa kula wa ya karne.
Kuhusiana
na viingilio alisema kuwa tiketi zitauzwa kwa shilingi elfu kumi na
kuongeza kuwa wanamuziki watakaoshiriki onyesho hili wamejipanga kutoa
burudani kisawasawa na kukata kiu ya wapenzi wa muziki wote Nchini.
Alisema
tiketi za onyesho hilo zitauzwa katika vituo mbalimbali Nchini yakiwepo
maduka ya Vodacom Tanzania,Pia zitapatikana kupitia huduma ya
M-Pesa,Katika kuwapunguzia washabiki usumbufu wa kupanga misururu ya
kununua tiketi za onyesho hilo pia zitauzwa kwa kupitia huduma ya M-Pesa
bila kuwepo na makato yoyote ya kutumia huduma hiyo ambapo watakaonunua
tiketi kwa huduma hiyo kutakuwepo na utaratibu maalumu wa kuingia
kwenye onyesho cha muhimu ni kutunza namba zao za kumbukumbu ya mhamala
wa malipo.Jinsi ya kujipatia tiketi kwa njia ya M-PESA mteja anatakiwa
kupiga *150*00# na kuchagua LIPA KWA M-PESA
Chagua MANUNUZI
Chagua JEMBEKA FESTIVAL
Weka namba ya kumbukumbu – 200200
Weka kiasi – 10,000
Weka Namba yako ya siri na kwa wale wa tiketi za VIP namba ya kumbukumbu ni 200100 bila malipo yeyote yale.
CREDIT:GPL
Post a Comment