Nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imechezwa Usiku wa May 4 2016 kwa klabu ya Real Madrid ya Hispania, kuwakaribisha Man City ya Uingereza katika nusu fainali ya pili iliyochezwa uwanja wa Santiago Bernabeu. Real Madrid imefanikiwa kutinga fainali kwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita Real Madrid walicheza ugenini katika uwanja wa Man City uitwao Etihad na mchezo kumalizika kwa sare ya kutofungana, lakini Real Madrid walicheza bila mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo ambaye mchezo wa leo alikuwepo. Goli pekee la Real limepatikana kwa Fernando kujifunga dakika ya 20.
Real Madrid wameingia uwanjani wakiwa wamewahi kufungwa na timu mbili kutoka Uingereza katika uwanja wao wa nyumbani, vilabu vya Uingereza vilivyowahi kuifunga Real Madrid Bernabeu ni Arsenal mwaka 2006 na mwaka 2009 wakafungwa tena Liverpool katika uwanja huo. Kwa sasa Real Madrid imefikisha jumla ya mechi 15 ilizocheza Bernabeu na vilabu kutoka Uingereza, imefungwa mara 2, sare mara 5 na wameshinda mara 8.
Video ya goli la Real Madrid vs Man City
Post a Comment