mechi kati ya Vijuso Fc Vs Wakaanga Sumu mchezo uliochwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano Liwale Mjini hii leo
Leo ikiwa May 4 katika Ligi ya Mbuzi vijana Cup inayoendelea hapa wilayani Liwale siku ya leo kulikuwa na mchezo wa aina yake katu ya VIJUSO Vs WAKAANGA SUMU mchezo uliotimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano.
Katika kipindi cha kwanza cha mchezo timu ya Vijuso ilikuwa ya kwanza kujipatia goli lililofungwa katika dakika 29 kupitia mchazaji wao Yuba Mmocha na dakika ya 38 wakaanga sumu waliweza kusawazisha goli kupitia mchezaji wao Muba na mapaka mapumziko walikuwa wamefungana moja kwa moja.
Kipindi cha pili kilianza kila timu walicheza mcheo mkali zaidi na wa kasi lakini timu ya Vijuso ilizidiwa na kasi hiyo ndivyo wapizani wao waliweza kutumia nafasi hiyo na kuweza kuongoza magoli 3,magoli ya Wakaanga sumu yaliyofungwa katika dakika 53 na Joti,dakiaka 65 mgosi na la tatu na la mwisho lilifungwa na Muba katika dakika 83 na mpaka mpira unamalizika 90 matokeo yalikuwa Vijuso 1-4 Wakaanga Sumu.
Kocha wa timu ya Vijuso fc, Ramadhani Milango alisema mchezo wa leo mzuri lakini tatizo ni kwa mwamuzi wa mchezo kutokana na kasoro ndogondogo za uchezeshaji nae kocha wa Wakaanga Sumu,Saidi Matongo alisema mchezo wa leo ulikuwa mzuri kwa upande wao na ameikubali timu ya Vijuso kwa uwezo wao wa uchezaji.
Kesho May 5 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya Kigamboni Vs Nangando mchezo utakaochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano Liwale Mjini.
Kesho May 5 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya Kigamboni Vs Nangando mchezo utakaochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano Liwale Mjini.
Post a Comment