MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Mh:Sospeter Nachunga
(aliyeshika kipaza sauti) akisoma Dua ya Halmashauri kabla ya kuanza kwa
kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo. Kushoto kwake ni mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Mh:Halima Dendego na Mkuu wa Wilaya ya Masasi
Mh: Bernald Nduta. Kulia kwake ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya
Mji wa Masasi Mh;Ausi Mnela,mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi
Fortunatus Mathew Kagoro na mkuu wa idara ya ukaguzi wa ndani mkoa wa
Mtwara. (Picha ya Maktaba)
TAARIFA
KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI:
BAJETI
YA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI 2016/2017
Bajeti
hii ya Halmashauri ya Mji wa Masasi ya Mwaka wa fedha wa 2016/2017 imeandaliwa kwa kuzingatia
vipengele vifuatavyo:
¨ Sheria ya Bajeti No: 11 ya mwaka 2015
¨ Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano awamu ya pili.
¨ Hotuba ya Rais wa awamu ya tano Mh:.John Pombe Magufuli ya Novemba 2015
¨ Ilani ya Uchanguzi ya CCM ya mwaka 2015.
¨ Vipaumbele vya Halmashauri vikihusisha
pia vile vilivyotoka ngazi ya Kata na Vijiji
Halmashauri ya mji wa
Masasi inatarajia kutumia fedha kiasi cha Tsh. billioni 19,092,007,820.00
MAPATO:
Katika fedha hizo:
Tsh. Billioni 1, 867,144,000.00 mapato ya ndani
sawa na asilimia 9.8.
Tsh. Biliioni 15,925,855,820.00
ni Ruzuku
kutoka serikali kuu sawa na asilimia 83.4 ya bajeti yote ya mwaka wa fedha 2016/2017.
Tsh. Billioni 1,299,008,000.00 ni
mchango kutoka kwa wahisani mbalimbali wa nje
sawa na asilimia 6.8 hivyo kufanya kuwa na jumla ya bajeti ya Tsh
Billioni 19,092,007,820.00.
MATUMIZI
Katika fedha hizo kiasi cha;
1. Tsh. Billioni
11,384,584,000.00 ni matumizi ya mishahara ya watumishi,ambapo ni sawa na
asilimia 59.6 ya bajeti yote.
2. Tsh. Billioni 4,808,636,820
ni fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 25.19.
Bajeti hii ya kiasi cha Tsh
billion 19,
092,007,820.00 kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 imeongezeka
kutoka ile ya mwaka Jana ya Tsh.
billioni 16,954,310,834.00 2015/2016 ambayo jumla ni sawa
na ongezeko la asilimia 12.6.
MCHANGANUO WA FEDHA ZA
MISHAHARA NA MATUMIZI YA KAWAIDA
Tsh. billioni 12,416,227,000.00
1. Tsh. 1,031,643,000.00 ni
matumizi ya kawaida (O.C)
2.
Tsh. Billioni 11,384,584,000.00 ni
mishahara.
MATUMIZI YA MAPATO YA NDANI YA TSH.1, 867,144,000.00.
1.Tshs. 764,359,000.00 sawa na asilimia
40 matumizi ya kawaida
2.Tsh. 186,714,000.00 sawa na asilimia 10 miradi ya Maendeleo ya Wanawake na Vijana.
3.Tsh. 933,572,000.00 sawa na asilimia 50 miradi ya Maendeleo.
MCHANGANUO WA FEDHA ZA MIRADI YA
MAENDELEO
Tsh billioni
4,808,636,820.00
1. Ruzuku (LG-CDG) Tsh. 418,485,000.00
2. Mfuko wa Barabara (Road
Fund) Tsh. 2,241,143,820.00
3. SEDP Tsh. 335,
484,000.00
4. Maji (RWSSP) Tsh. 179,513,000.00
5. TASAF Tsh. 579,447,000.00
6. Mfuko wa
pamoja wa Afya (Basket Fund) Tsh. 204,564,000.00
7. Maombi
Maalumu
¨
Jengo la utawala Tsh.750,000,000.00
¨
Miundo mbinu shule maalumu Tsh.100, 000, 000,
00.
MCHANGANUO WA FEDHA KUTOKA
SERIKALI KUU TSH: BILLIONI 15,925,855,820.00
sawa na asilimia 83.4.
1. Tsh 11,384,584,000.00
-mishahara ya watumishi
2. Tsh 1,031,643,000.00 matumizi
ya kawaida
3. Tsh3, 509,628,820.00 fedha za miradi ya Maendeleo
kutoka serikali kuu
5. Tsh 1, 299,008,000.00 ni fedha kutoka kwa wahisani wa
maendeleo wa nje.
BAJETI
HII IMETOA VIPAUMBELE 07 2016/2017 AMBAVYO NI:
a)
Kuwezesha upatikanaji wa elimu bora ya msingi na sekondari kwa kuzingatia usawa
b)
Kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya pembezoni mwa
halmashauri.
C)
Kuboresha usafi wa mazingira hasa katika maeneo yenye msongamano kama Kituo cha
mabasi na sokoni.
d)
Kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya Halmashauri na kudhibiti matumizi
ya fedha za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.
e)
Kurasimisha makazi yasiyo rasmi na kuongeza kasi ya upimaji viwanja kwa ajili
ya makazi,biashara,viwanda na maeneo ya kuabudia.
g)Kuongeza
wigo wa ajira na kuboresha hali ya usalama
wa kijamii (socio- Protection) hasa kwa wanawake , vijana, makundi maalumu,
wazee na watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.
h)
Kukarabati miundombinu ya barabara za Halmashauri
MWISHO:
Aidha katika Makisio ya Mpango na
Bajeti ya Mwaka 2016/17 Halmashauri ya mji wa Masasi imejikita katika kutekeleza azma ya serikali ya kutoa elimu ya
msingi na sekondari bila malipo kwa kufanya mambo yafuatayo:
·
Kulipa
likizo kwa walimu
·
Kugharamia
Chakula mashuleni
·
Kulipa
gharama za uhamisho kwa walimu
·
Uendeshaji
wa ofisi
·
Gharama
za mitihani.
Imetolewa na Kitengo Cha Habari na Mahusiano,
Halmashauri ya Mji wa Masasi,
25 April, 2016.
Post a Comment