Rashford kusalia Man United hadi 2020
Mshambulizi
chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford ametia sahihi mkataba
mpya utakaohakikisha anasalia Old Trafford hadi Juni 2020.
Chipukizi
huyo mwenye umri wa miaka 18 amekonga nyoyo za wafuasi wa Manchester
United tangu alipoisaidia timu yake kuizaba Midtjylland katika mechi
yake ya kwanza mwezi Februari.Rashford ameichezea Man United katika mechi 18 na kuifungia mabao 8.
Rashford amejiunga na timu ya England itakayoshiriki katika michuano ya Euro 2016.
Ijumaa iliyopita talanta yake ilingaa zaidi alipofuma bao la kwanza la kimataifa dhidi ya Australia.
Kijana huyo anakisiwa kuwa analipwa takriban pauni £20,000 kwa Juma.
Naibu mwenyekiti wa Manchester United bwana Ed Woodward alimmiminia sifa kedekede chipukizi huyo
''bado ni kijana sana huyo kwa hivyo tunahitaji kumpa muda zaidi iliakomae kitaaluma , kwa sasa tunashuhudia akinoa makali yake na bila shaka atakuwa mchezaji nyota katika siku za usoni''
Post a Comment