SURA YA NNE.
Nilipiga hatua kadhaa baada ya kutoka ndani kwangu hatua ambazo hazikuchukua
muda mwingi hatimaye nilikuwa nimefika uwanjani lakini cha ajabu sasa
nilishangaa hali niliyokutana nayo pale kiwanjani.
____________
Sasa saba usiku zilisikika sauti ambazo zilikuwa zikiongozwa na mganga Mzazu
huku akiwa pamoja na viongozi wa kijiji.
“Hahahahaha….tulia” Sauti ya Mzazu ilisikika huku akiwa ameshika kitu
mithiri ya pembe la ngo’mbe akirizungusha zungusha kwa muda kidogo.
Kabla hajanena kitu mbele ya viongozi wa kijiji kile wakiwa wanaongozwa na Mwenyekiti, Baba Jack.
Kabla hajanena kitu mbele ya viongozi wa kijiji kile wakiwa wanaongozwa na Mwenyekiti, Baba Jack.
“Naam! Tatizo lenu nimelitambua, hahahaha! nimelitambua” Sauti ya
kutetemesha na kuogofya ilitoka ndani ya kinywa cha Mzazu na kuwaogopesha zaidi
viongozi wale.
Wakati huo kijiji kilikuwa tuli, kimya kilikuwa kimetawala kumwachia Mzazu.
Walikuwa wakiona kama mkombozi wao kutokana na kadhabu walizokuwa wakizipata
kutoka kwa Mzee Shabani, gwiji la wachawi.
“Leo ndio mwisho wake, nimeamua kumalizana nae, lakini kabla sijalimaliza
ili lazima mtambue kitu kimoja Mwenyekiti,” aliita Mzazu kwa sauti iliyomfanya
kumshtua Baba Jack. “Sikia, wewe na Mzee Shabani mlikuwa mna matatizo wa
uongozi, kumbuka wakati mnaitisha uchaguzi wewe ukiwa kiongozi ambaye uliamua
kugombea tena. Wakati huo Mzee Shabani akiwa na miezi mitatu ndani ya kijiji
lakini alikuwa akipendwa sana na hata alipoamua kugombea kwenye uchaguzi ule na
kushinda, ila nyinyi kutokana na fitina zenu mliamua kupindisha lile, na hata
alipoamua kuwafata kistarabu mlikuwa mkijibu majibu yasiyoridhisha, hahahahaa.”
Mzazu aliongea maneno yale yaliyofanya kuwatisha zaidi viongozi wa kijiji.
“Hahaha… lakini Mzee Shabani ni mtoto mdogo kwangu, leo ndio nataka mtambue
kwanini niliitwa kiboko ya Wachawi wote, leo ndio mwisho.” Mzazu aliongea huku
akifikicha macho yake kabla ya hali ya eneo lile kubadilika na kuwa sehemu ya
ajabu sana.
Taswira za wale viongozi vilionana ana kwa ana na Mzee Shabani, wakati huo
mpambano mkali ulizuka baina ya Mzazu na Mzee shabani, mpambano ulidumu zaidi
ya nusu saa. Kabla ya Mzee Shabani kukimbia eneo lile, sekunde kadhaa zilianza
kusikika sauti za vilio kutoka kila sehemu ya kijiji cha Tangeni, vilio ambavyo
havikuwa vya kawaida huku eneo lile ambalo lililogeuka uwanja wa vita
kilisikika kicheko kikali.
“Hahahahaha.” Kicheko ambacho kilimpagawisha Mzazu kabla ya kukaa sawa na
sauti zile za vilio kupenya sawia kwenye masikio ya Mzazu na viongozi wa
kijiji.
Kazi ilikuwa ngumu sana kwa upande wao maana licha ya jitihada ambazo Mzazu alizifanya usiku kucha bado hakuambulia tena kudhibiti Mzee shabani ambaye asubuhi aliacha vilio na simanzi ndani ya kijiji haswa kwa koo za viongozi walikuwa wamekufa karibia watu wote ndani ya koo zao. Hiyo iliongeza machungu sana haswa kwa Baba Jack ambaye alipoteza ndugu zake wote.
Kazi ilikuwa ngumu sana kwa upande wao maana licha ya jitihada ambazo Mzazu alizifanya usiku kucha bado hakuambulia tena kudhibiti Mzee shabani ambaye asubuhi aliacha vilio na simanzi ndani ya kijiji haswa kwa koo za viongozi walikuwa wamekufa karibia watu wote ndani ya koo zao. Hiyo iliongeza machungu sana haswa kwa Baba Jack ambaye alipoteza ndugu zake wote.
Ajabu zaidi hakufanikiwa kuona mwili wa mkewe kipenzi Mama Jack jambo ambalo
lilizidi kumwongezea machungu dhidi ya Mzee shabani. Wakati huo mchana kutwa
Mzazu akitathimini njia gani ya kumthibiti Mzee Shabani.
________
Uwanja ulikuwa umefurika kila sehemu huku shangwe zilikuwa zikisikika sawia
ndani ya masikio yangu shangwe ambazo dhahiri zilikuwa kutokana na kile
kilichokuwemo uwanjani mule. Ugeni ule ulinishangaza zaidi lakini nilijijibu
mwenyewe kutokana na kushindwa kuhudhuria uwanjani pale kwa siku mbili ndio
maana nilikuwa sijapata taarifa za mechi ile ambayo ilikuwa ikituhusisha timu
yetu ya kijiji na timu ile ya kijiji cha Misongeni.
Niliendelea kuangalia mechi ile nikiwa nafatilia kila tukio lilikuwa
likiendelea pale kwa mbali upande wa pili macho yangu yalionana na Mwajabu.
Kiuzuri yeye pia alikuwa ameniona kuonana kule kulienda sambamba miguu yangu
kujongea mahali kule alipokuwa amekaa Mwajabu.
Sikuchukua dakika nyingi nilikuwa nimefika eneo lile na kuanza kuzungumza na
Mwajabu huku watu walikuwa karibu yetu walitega vyema masikio yao kusikiliza
kile tulichokuwa tunaongea. Mechi nayo ilikuwa ikiendelea na wakati huo bado
matokeo yalikuwa vile vile kama nilivyokuwa nimeyakuta. Nilimuuliza Nyumbani
vipi akaniambia alimkuta Baba yake anajiandaa kuja kuangalia mechi ile ila
akuongea sana hivyo waliongozana wote kuja eneo lile.
Maneno yake yalinitisha kumbe muda wote tunaongea Mzee shabani alikuwa eneo lile, wakati natafuta neno la kuongea juu ya lile ile nageuka macho yangu yaligongana na ana kwa ana na Mzee Shabani.
Maneno yake yalinitisha kumbe muda wote tunaongea Mzee shabani alikuwa eneo lile, wakati natafuta neno la kuongea juu ya lile ile nageuka macho yangu yaligongana na ana kwa ana na Mzee Shabani.
Kwanamna ya uangaliaji alikuwa ananingalia nilijuwa wazi atakuwa anakitu
anafikiria juu yangu hivyo neno lilofatia kwenye kinywa changu ni kumuaga tu
Mwajabu, wakati huo nikiwa nachepuka kutafuta mahali kwa kukaa sikutaka Mzee
shabani anione tena naongea na mwanae.
Nilirudi eneo lile nilipokuwa naangalia mechi ile kwa mara ya kwanza lakini
hali haikunipa kabisa, kupenda kwangu mpira kote lakini siku ile ilinishinda
kabisa. Nilijikuta tu miguu yangu inanisukuma na kuongoza njia ya kwenda
Nyumbani. Muda nao ulikuwa umeenda kijua taratibu kilianza kupotea kuukaribisha
usiku wa siku hiyo.
Nilifika Nyumbani nikafanya taratibu za kula mapema tu, nilipika chakula na
kula mpaka pale nilipoona nimetosheka, niliamua kujitupia kitandani kwa muda
kidogo. Mambo yale ya mchana yalikuwa yakijirudia rudia ndani ya kichwa changu.
Yalicheza kweli kwenye kichwa changu kwa muda hatimaye usingizi ulinichukua.
“Mwanangu Jack, achana na yule Mwanamke utajisababishia matatizo makubwa
sana. Baba yake si mtu mzuri. Najua jinsi gani mnavyopempenda na hata wewe
unampenda lakini kuna shida sana ndani ya penzi lenu.”
“Shida gani Mama wakati tunapendana, najua kuwa amechumbiwa lakini yeye
alinimbia mwenyewe kwa kinywa chake kuwa hatakubaliana na hilo Mama.”
“Nalijua hilo lakini wewe hujui jinsi gani yule Mzee wake alivyosabisha
machungu upande wako, yuko wapi Mjomba wako? Yuko wapi Baba yako? Yote kwa jili
yake na wewe unataka kuwa kama wao?”
Maneno ya Mama yalisikika vyema kwenye masikio yangu wakati nipo usingizini. Yalinistua sana. Niliogopa mno.
Maneno ya Mama yalisikika vyema kwenye masikio yangu wakati nipo usingizini. Yalinistua sana. Niliogopa mno.
“Ahhhh! Imekuwaje hili?” Nilijikuta nikjisemea mwenyewe wakati huo nikiwa
nahema mithili ya saa iliyopoteza majira.
“Aaaaaa! Kwanini? Inamaana gani?” Hapo hata usingizi haukuja tena.
Si sauti ya Mama yangu ilikuwa ikiyanena yale maneno wakati nipo usingizini,
inawezekana vipi? Nilijiuliza kwa mara nyingine. Hapo ilinikumbusha mbali sana
Vifo vya wazazi wangu ambavyo vilitokea kiutata utata na hata mazishi yake
sikupata kuhudhuria mimi wala Mjomba. Nilikumbuka kile kilichotokea miaka
mitatu nyuma ndani ya kijiji cha Tangeni.
Vifo vilivyokuwa vikihusishwa na uchawi. Nikiwa kwenye kitanda changu ghafla
zilisikika hatua kama za watu zinatembea ndani ya juu ya paa la chumba changu
jambo ambalo liliniogopesha sana pale kitandani. Hatua zile zilichukua muda
kadhaa kabla ya kupotea masikioni mwangu.
Nilitulia pale nikitafakari jambo lile. Kufikiria kule hata sikuelewa
nilijishangaa tu macho yangu yanafumba na kulazimishwa kuingia kwenye usingizi,
usingizi ambao haukuwa wa bure kabisa, ninaweza kusema maana mambo ya ajabu
sana niliyoona ndani ya usingizi ule. Alikuwa ni Mzee Shabani kabisa kwenye mboni
za macho yangu huku akijitahidi kufanya kitu ambacho wazi niliona akishindwa,
kila alipojaribu kunisogelea hakuwa pekee yake alikuwa na gwiji la wachawi
ndani ya kijiji chetu Bibi Subira na wachawi wengine wakiwa uchi kama
walivyozaliwa. Sura zao zilikuwa kama na masizi hivi lakini mboni zangu
ziliweza kutambua lile.
Walikuwa wakicheza mbele na kurudi nyuma kimgongo mgomgo, nilikuwa nikiogopa
mno. Kila nilipokuwa nikiwatazama na mimi kunitazama. Nilisikia vijimaneno vyao
ambayo yalinitisha zaidi ya kwamba wazazi wangu aliweza kuwamaliza kiurahisi
mimi nimekuwa mgumu eti lazima ale sahani moja na mimi.
Upepo mkali ulivuma wakati huo bado nikiwa naangalia kile nikiwa kwenye
usingizi ule wa kulazimishwa, huku nikijitahidi kufumbua macho na kunyanyua
mdomo wangu kupiga yowe la kuomba msaada, lakini ile ilikuwa kama kujisumbua tu
mdomo ulikuwa mzito kufanya vile. Mwanga mkali ulinijia ndani ya mboni zangu na
kujenga taswira nyingine.
Post a Comment