0

Maofisa Elimu wawili katika Halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wamevuliwa madaraka yao kwa kosa la kuridhia michango ya wanafunzi katika baadhi ya shule wilayani humo,jambo ambalo ni kinyume cha agizo la Rais Dk. John Magufuli la kutaka wanafunzi wote wapate elimu bure.
Agizo la kuvuliwa madaraka kwa maofisa hao wawili wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali ambao ni Afisa Elimu ya msingi,Henerico Batinoluho na Afisa Elimu ya msingi taaluma,Michael Chaula limetolewa na Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo baada ya kukaa kama kamati ya nidhamu ya watumishi na kuwajadili kabla ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Jeremeah Mahinya kutoa tamko la azimio hilo kwa umma.
 
Kwa upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Mbarali,Gullam Hussein Kifu akasema kuwa serikali ya awamu ya tano inahitaji uwajibikaji,hivyo akawaonya watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawajibike ipasavyo kutoa huduma bora kwa wananchi.

Post a Comment

 
Top