Mwanamke
mjamzito ameokolewa kutoka vifusi vya jengo lililoporomoka jijini
Nairobi baada ya kuwa chini ya vifusi vya jengo hilo kwa siku sita tangu
jengo hilo kuporomoka ijuma usiku.
Siku mbili zilizopita Wakenya walishangazwa na tukio la mtoto wa
miezi sita kuokolewa kutoka kwa vifuzi vya jengo lililoanguka mtaa wa
Huruma jijini Nairo na mapema leo mshagao zaidi umewapata baada ya
mwanamke mjamzito kuokolewa kwenye vifusi hivyo.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya linasema mwanamke huyo
yumo katika kali nzuri licha ya kupata uchofu na kukosa chakula kwa siku
sita alizokuwemo ndani ya vifusi vya jengo hilo.
Kwa mujibu wa Pius Masia Mkuu wa Kitengo cha kukabiliana na maafa
nchinihumo amesema matumaini yakupata manusura wakiwa hai yanazidi
kuongezeka.
Kufikia sasa idadi ya waliofariki kutokana na ajali hiyo imefikia
watu 36 huku watu 80 wakiwa hawajulikani waliko hadi sasa na watu 138
wakiwa wameokolewa.
Mamlaka inayosimamia shughuli za ujenzi nchini Kenya imesema mpango
wa kubomoa majengo 200 ambayo hayajatimiza sheria na masharti ya ujenzi
utaanza mapema juma lijalo.
Post a Comment