Hukumu
hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha baada ya washtakiwa kukiri kosa. Washtakiwa
waliohukumiwa kifungo hicho ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Feng Shi
Trading, Sun Ning (39) na Fen Quan (51).
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema washitakiwa wamepatikana na hati ya
makosa matatu, na kwa kosa la kwanza kila mmoja atalipa faini ya Sh
milioni 10 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela, kosa la pili
faini ya Sh milioni 20 au jela miaka mitano, kosa la tatu faini ya Sh
milioni 20 au jela mwaka mmoja.
Alisema
kwa makosa yote, adhabu yao ni sawa na kifungo cha miaka 11 jela au
kila mmoja kulipa faini ya Sh milioni 50, lakini adhabu ya kifungo
inakwenda sambamba hivyo ni sawa na kifungo cha miaka mitano jela.
Hakimu
Mkeha alisema ametoa adhabu hiyo kwa kuzingatia kuwa, washtakiwa ni
wakosaji wa mara ya kwanza na wamekuwa na ushirikiano mzuri kwa kukiri
makosa yao kwa madai walikuwa hawajui kama ni kosa.
Aidha
alisema kwa sababu fedha hizo hazijafanikiwa kuhamishwa na zilikuwa
fedha halali za washtakiwa hao, aliamuru Sun arudishe fedha zake Sh
milioni 20. Katika mashtaka yao inadaiwa kati ya Agosti 15 na 31 mwaka
jana, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Ilala Dar
es Salaam, washtakiwa hao walisafirisha noti 10,000 za Sh 500 zenye
thamani ya Sh milioni tano kwenda China bila kibali kutoka kwa gavana.
Aidha
wanadaiwa kati ya Desemba 22 na 31 mwaka jana wakiwa uwanjani hapo,
walisafirisha noti 10,000 za Sh 500 zenye thamani ya Sh milioni tano
bila kibali, pia walikutwa wakisafirisha noti 40,000 za Sh 500 za
thamani ya Sh milioni 20 kwenda China bila kibali.
Baada
ya kusomewa mashitaka hayo, washtakiwa hao walikiri kutenda kosa hilo
na kusomewa maelezo ya kesi ambapo ilidaiwa kwamba Sun ambaye ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Feng Shi Trading aliingia nchini Machi 13 mwaka
huu.
Kwa
mujibu wa maelezo ya awali, Machi 10 mwaka huu Feng alitoa noti za 500
zenye thamani ya Sh milioni 20 kutoka kwenye akaunti yake namba
015240837900 CRDB Tawi la Kariakoo.
Ilidaiwa
baada ya kuchukua fedha hizo, Sun alimpa Feng dola za Marekani 8,120 na
yeye kumpa fedha hizo za Kitanzania na Machi 14 mwaka huu Feng
aliingiza dola 8000 katika akaunti yake ya fedha za kigeni iliyopo benki
ya CRDB.
Machi
16 mwaka huu Feng alimsindikiza Sun uwanja wa ndege akisafiri kwenda
nchini China lakini wakati wa ukaguzi alikamatwa akiwa na kiasi hicho
cha fedha akikisafirisha bila kibali.

Post a Comment