0



Abiria zaidi ya 300 wanaosafiri kutoka Liwale mkoani Lindi na wanaoelekea wilayani humo kutoka Dar es Salaam na maeneo mengine wamekwama kwa siku mbili njiani kufuatia ubovu wa barabara kuu inayoingia wilayani humo kuanzia Nangurukuru kufuatia magari kukwama kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini na hivyo kusababisha adha kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Wakizungumza na ripota katika eneo la Zinga Kibaoni baadhi ya wasafiri hao wamesema kuwa barabara hiyo imekuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa Liwale ambapo katika kipindi cha mvua imekuwa ni kawaida kulala njiani huku nauli zikiwa juu na wamiliki wa magari kusitisha safari na hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa. 
Baadhi ya madereva wa magari yaliyokwama wakizungumzia tatizo hilo wamesema kuwa changamoto ya barabara hiyo imekuwa ikiwagharimu sana  na wamiliki nao wamekiri ya kwamba magari yanatumia  gharama kubwa wanazotumia katika kutengeneza magari yao na hivyo kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutengeneza barabara hiyo kutokana na umuhimu wake. 
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Liwale Gaudence Nyamwihura akizungumzia na waandishi wa habari amekiri kuwepo kwa taarifa hiyo ambapo kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya Bw.Ephraim Mmbaga wamekwisha anza kuchukua hatua za tahadhari kwa kuwashirikisha wakala wa barabara nchini Tanroads ili kunusuru hali hiyo.
           >>>ANGALIA PICHA ZINGINE KWA KUBOFYA HAPA  

Post a Comment

 
Top