|
MWENYEKITI
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kagoli amefikishwa
mahakamani kwa kosa la kuhifadhi wahamiaji haramu nyumbani kwake na
kuwatumikisha mashambani.
Kagoli
ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kageji, anakabiliwa na mashitaka matatu
ikiwemo kuishi na watu ambao sio raia, kuwasaidia raia wa kigeni kutenda
kosa na kuajiri na kuwatumikisha wageni shambani mwake. Kesi hiyo namba
114/2016 iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo, Robert
Male.
Mwendesha
Mashitaka wa Uhamiaji, Richard Mwangole alidai mshtakiwa alitenda kosa
hilo kwa makusudi huku akijua kuwa kuhifadhi wahamiaji haramu ni kosa
kubwa. Anatuhumiwa kuwafanyisha kazi wahamiaji hao na kuwalipa ujira wa
Sh 110,000 kila mmoja. Male alikana makosa na yuko nje kwa dhamana.
Alidhaminiwa na wadhamini wawili, kila mtu kwa dhamana ya Sh milioni moja.
Post a Comment