Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akionyeshwa na kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamla ya
bandari Tanzania, Mhandisi Aloys Mtei eneo zinakotia nanga meli kubwa
zinazoleta mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es salaam Februari 11,
2016. (Picha na ofisi ya Waziri Muu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Vipimo na Mizani, Bibi Magdalena Chuwa (kulia) kuhusu sababu
zilizomfanya azuie matumizi ya flow Meter katika kuhakiki kiwango cha
mafuta yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es salaam wakati
alipofanya ziara kwenye badari hiyo Februari 11, 2016. katikati ni Mkuu
wa Wilaya ya Ilala,Raymound Mushi. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo ambalozo mafuta hufunguliwa na
kufungwa ili kwenda kwenye matangi ya kuhifadhia mafuta ya makampuni
mbalimbali yanayoagiza mafuta toka nje ya nchi wakati alipokwenda enero
la Kigamboni jijini Dar es salaam kuonamianya inayotumika kukwepa kodi
za mafuta yanayoagizwa nje ya nchikupitia bandari ya Dar es
salaamFebruari 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua flow Meter ya Mafuta ya kupikia ambayo
matumizi yake yalizuiwa na Wakala wa Vipimo na Mizani kwa madai kuwa
ilikuwa na kasoro . Wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakla wa Vipimo na
Mizani, Magdalen Chuwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WaziriMkuu,
Kassim Majliwa akikagua ujenzi wa Flow Meter eneo la Kigamboni jijini
Dar es salaam Februari 11, 2016. Mtambo huo utatumika kupima wingi
wamafuta yanayotoka kwenye meli na kuingizwa hapa nchini. Kulia kwake ni
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymound Mushi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo lenye mabomba yanayotumika
kupitisha mafuta kutoka kwenye meli kupitia bandari ya Dar es slaam
wkatia lipofanya ziara ya kukagua miundombinu yenye mianya ya ukwepaji
kodi hasa kwenye mafuta yanayoingia nchini Februari 11, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Aibukia kitengo cha mita za kupimia mafuta Kurasini
*Akuta mafundi wakizitengeneza, akuta zimejaa kutu
*Ataka barua ya maelezo ifikapo saa 11 leo jioni
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya ghafla kwenye kitengo cha
upimaji mafuta bandarini (Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada
ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano. Pia alitembelea mita za
kupimia mafuta zinazoendelea kujengwa Kigamboni.
Aidha,
Waziri Mkuu amempa saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini
(WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini
aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita
na amletee barua hiyo ofisini kwake ifikapo saa 11 leo jioni.
“Nataka
unieleze ni kwa nini ulitoa maelekezo ya kufunga mita hizo, na kwa nini
jana uliamua kubadili uamuzi huo? Ni kwa nini umeamua kuchukua maamuzi
haya baada ya kupokea ujumbe wa simu ya mkononi (sms) wakati mita
zimekaa bila kufanya kazi kwa miaka mitano? Ni kwa nini umeamua kufanyia
kazi ujumbe wa sms wakati unajua Serikali inafanya kazi kwa maandishi
rasmi?” alisema Waziri Mkuu.
“Umesema
mlikuwa mnatumia utaratibu wa kupima kwa kijiti. Huu hauna uhakika na
huwezi kutegemea taarifa ya mtu mwingine au kuingia kwenye meli ya mtu
na kuanza kuchukua vipimo hadi ujiridhishe. Nataka kujua ni kwa nini
mlikuwa na utaratibu wa ku-bypass mafuta ili yasipite kwenye mita za
kupimia mafuta? Ni kwa nini umetoa amri zianze kutengenezwa jana na siyo
mwaka 2012 au 2013?” alihoji Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu alisema mita hizo za Kurasini zilinunuliwa na Serikali kwa gharama
za dola za marekani milioni 1.2 (wakati huo) na haiwezekani kuacha
kuzitumia wakati watu wanachezea mifumo na kuongeza mianya ya kupoteza
mapato kwa Serikali. Ameagiza mita hizo zianze kufanya kazi mara moja.
Wazir
Mkuu alisema matumizi ya mita hizo yaliafikiwa na Serikali baada ya
kubaini upotevu mkubwa wa kodi kwenye mafuta yanayoingizwa nchini na
baada ya kuona hakuna tija ya kuendelea na ukadiriaji au kupokea taarifa
za waagizaji peke yao.
Waziri
Mkuu ambaye aliwasili Kurasini leo saaa 4: 30 asubuhi (Alhamisi,
Februari 11, 2016) kwenye kitengo hicho kilichopo Kurasini (Kurasini Oil
Jetty), alikagua mita hizo na kisha kwenda kukagua meli iliyokuwa
ikishusha mafuta bila kutumia mita hiyo ya kupima mafuta yanayopokelewa
kwa sababu mafundi walikuwa bado wanaendelea na ukarabati.
Akiwa
Kurasini, Waziri Mkuu alielezwa na Bibi Chuwa kwamba mita hizo zilianza
kufanyiwa ukarabati jana na leo asubuhi moja imekamilika ambayo ni ya
kupokelea mafuta ya petroli. Ya dizeli ilikuwa inafunguliwa na mafundi
na kukutwa imejaa kutu sababu ya kutotumika kwa muda mrefu.
“Hii
ya dizeli imefunguliwa leo na ile ya mafuta ya kula, haijawahi kufanya
kazi tangu ilipofungwa mwaka 2011,” alielezwa Waziri Mkuu na Kaimu
Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei.
Alipoulizwa
ni kwa nini aliamua kuzifungia mita hizo ziisifanye kazi, Bi. Chuwa
alijibu kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kwamba
zinawapunja wateja. Hata hivyo, hakufafanua ni wateja gani au wa aina
gani.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea na kukagua mita mpya
za kupimia mafuta ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu
dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).
Akiwa
hapo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba ujenzi huo ambao ulianza miezi nane
iliyopita, unatarajiwa kukamilika ifikapo katikati ya mwezi Machi, 2016.
“Tunajitahidi kazi hii ikamilike ifikapo katikati ya mwezi ujao,”
alisema Eng. John Bura, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya BQ Contractors
Ltd ambayo inasimamia ujenzi wa mita hizo.
Vilevile,
Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka
bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya
kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko
Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia bainaya Serikali na kampuni ya Oryx
Energies.
Katika
ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la
moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini
hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye
maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.
“Natoa
mwezi mmoja hili bomba liondolewe kwenye mfumo huu na kama yapo mabomba
mengine pia yaondolewe,” alisema huku akionyesha karatasi iliyokuwa
mfukoni kwake yenye mchoro unaobainisha kuwa kuna bomba jingine la inchi
10 limeungwa kinyemela kwenye bomba kuu.
“Kila mmoja anapaswa aje kuchukua pale kwenye manfold ili
tujue nani kachukua nini. Msajili wa Hazina hili ni eneo lako na wewe
unamiliki TIPER kwa asilimia 50, hebu simamia hili. Ninyi TPA leteni
mapendekezo yenu Serikalini ili tuone tunaweza kudhibiti vipi vitendo
kama hivi,” alisema Waziri Mkuu.
Pia
alimtaka Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru awasiliane na
Mwanasheria Mkuu ili waangalie upya mkataba na umiliki wa matenki hayo
uwe chini ya Serikali kwa asilimia 100 ili mafuta yanayoagizwa na Wakala
wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency)
yaweze kuhifadhiwa huko.
Mapema, Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alikagua eneo lamanfold ya Mamlaka ya Bandari iliyopo Kigamboni na kukuta ni kampuni nne tu zenye matenki Kigamboni ambazo zinachukua mafuta yao hapo.
Kampuni
hizo ni HASS, WORLD OIL, LAKE OIL na MOIL. TIPER haikutaka kufuata
mfumo huo licha ya kuwa nafasi ya kufanya hivyo ipo. Kampuni nyingine
zenye matenki yake nchi kavu, zinachukulia mafuta kwenye manfold ya Kurasini.
Post a Comment