0


 KAIMU meneja wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Kanda ya Kusini (TFS) Helbet Haule akiwaonesha waandishi wa habari (Hawapo Pichani) msumeno wa moto maarufu (Chain Saw) iliyokamatwa na kikosi cha operesheni maalumu.
Na Clarence Chilumba, Masasi.

Kukithiri kwa vitendo vya matumizi ya uvunaji wa misitu kwa kutumia misumeno ya moto (chain saw) kunakofanywa na wavunaji haramu wa misitu kanda ya kusini ndio chanzo kikuu cha uharibifu mkubwa wa misitu iliyopo mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.


Hayo yalisemwa jana wilayani Masasi mkoani Mtwara na kaimu meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)kanda ya kusini,Helbet Haule alipokuwa akizungumza na gazeti hili ofisini kwake kuhusiana na tatizo la kukithiri kwa uvunaji haramu wa misitu katika mikoa ya kanda ya kusini.

Alisema tatizo la uvunaji haramu wa misitu kanda ya kusini ni tatizo kubwa linalochangia kuharibu misitu iliyopo katika mikoa ya kanda ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.


Alisema wavunaji haramu wamekuwakitumia misumeno ya moto kukata miti kwenye hifadhi za misitu kwa ajili ya kupasua mbao kisha kuzisafirisha sokoni kwa njia ya panya jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za nchi na kwamba wanatakiwa kufuata sheria za uvunaji misitu.


Haule alisema TFS imejiwekea mkakati kabambe wa kufanya msako wa kuwakamata wavunaji wote haramu wa misitu katika mikoa hiyo pamoja na vifaa vyao wanavyotumia kukata miti ikiwemo misumeno hiyo ya moto ili kukomesha vitendo hivyo.

“Tunatoa agizo uvunaji wa misitu usiofuata kanuni na sheria ni kuvunja sheria hivyo kila anayetaka kuvuna misitu au kusafirisha mbao lazima afuate sheria husika za kufanya hivyo kwa kupata kibali maalumu,”alisema Haule

Alisema kwa kufanya doria shirikishi wamefanikiwa kukamata misumeno ya moto zaidi ya 32 inayotumiwa na wavunaji hao pia wamekamata misumeno ya kawaida ya kuchania mbao 10 magnia ya mkaa 41 yenye jazo wa kilogramu 12 pamoja na baiskeli 30 zinazotumika kubebea vipande vya mbao.


Aidha,Haule aliongeza kuwa TFS imekamata vipande vya mbao ambavyo vilikuwa vikisafirishwa kwa njia haramu zaidi ya 2,425 jamii inapaswa kutambua umuhimu wa kanuni na sheria za biashara ya mazao ya misitu ili waweze kufuna kwa miongozo ya kisheria iliyopo nchini.


Haule alisema miti aina ya Mpingo pamoja na Mninga imekuwa ikikatwa kwa kiasi kikuwa kutoka na miti hiyo kukuwa na thamani kubwa hivyo hifadhi nyingi za misitu katika kanda ya kusini iliyo na miti ya aina hivyo hutoweka kwa kuvumamiwa na wavunaji hao haramu.


Aliongeza kuwa wamefanikiwa kudhibiti vivuko vilivyoko katika kijiji cha Mtambaswala ambavyo vilikuwa vikitumika kuvusha mbao kwa njia haramu ikiwemo zile zinazotoka katika nchi ya jirani ya Msumbiji na kuingiza nchini kwa ajili ya kwenda kuuza katika mikoa mbalimbali.
 Baadhi ya shehena ya Mbao zilizokamatwa na ofisi ya wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Zikiwa katika makao makuu ya ofisi hiyo wilayani Masasi.
 Lori likiwa limekamatwa kwa kusafirisha mbao kinyume na utaratibu uliowekwa na TFS wilayani Masasi.
 KAIMU meneja wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Helbet Haule akiwaonesha waandishi wa habari lori lililokamatwa kwa kusafirisha mbao kinyume na taratibu.
Baiskeli zikiwa zimekamatwa ambazo zinahusika na usafirishaji wa mbao na Mkaa kinyume na taratibu zilizowekwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania.

Post a Comment

 
Top