
Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Wingi
wa vizuizi vya ukaguzi barabarani umetajwa kusababisha rushwa na
usumbufu kwa wafanyabiashara wanaosafarisha mazao ya misitu.
Hayo
yalielezwa jana na wafanyabiashara wa mbao na magogo kwenye warsha ya
wafanya biashara wa mbao na magogo wa uwanda wa Selous hadi Ruvuma,
iliyofanyika jana katika manispaa ya Lindi.
Wakizungumza
kwenye warsha hiyo iliyoandaliwa na mashirika ya kiraia ya Jumuiko la
Maliasili Tanzania(TNRF), Mtandao wa Kijamii wa Usimamizi wa
Misitu(MJUMITA) uhifadhi, usimamizi na maendeleo ya mpingo(MCDI) kupitia
kampeni ya mama misitu inayofadhiliwa na serikali ya Finland kupitia
ofisi za WWF zilizopo nchini, walisema vizuizi hivyo vinasababisha
rushwa, usumbufu na kuwapotezea muda.
Frank Nganyanyuka alisema wingi wavizuizi unasababisha wafanyabiashara hao kupoteza muda mwingi barabarani.
Alisema kutoka Nachingwea hadi Dar-es-Salaam kuna vizuizi takribani 19, ambavyo vinasababisha wachelewe barabarani
"Wastani
kila eneo lenye kizuizi tunatumia saa moja, maana yake siku mzima
inakwisha kwa ajili ya kusimama, vizuizi vipunguzwe havinafaida zaidi ya
kuchochea rushwa tu," alisema Nganyuka.
Mfanyabiashara
Mikidadi Kinogeandanga wa Lindi, alisema licha ya kuchelewa lakini pia
maofisa waliopo katika vizuizi hivyo niwasumbufu na hawaziamini nyaraka
ziliandikwa na maofisa wenzao wa kule zilikotoka mbao na bidhaa nyingine
za misitu. Alihoji nisababu gani zinazosababisha wasiwaamini wenzao
ambao wanadhamana na mamlaka kama yao.
Alibainisha
ili kuepuka kuchelewa wanajikuta wanarahisha usumbufu kwa kutoa
chochote, kwa madai bila kufanya hivyo wanasumbuliwa hata kama
hawakiuki, sheria, taratibu na kanuni.
"Malendego, Jaribu, Kimanzichana sijui wapi, niusumbufu tupu, lakini yote hayo nikutaka rushwa tu," alisema Kinogeandanga.
Ali Kinunga anayefanyia biashara yake wilayani Kilwa, licha kuyalalamikia wingi wa vizuizi alilaumu serikali kutowashirikisha wafanyabiasha wa mazao ya misitu ili kupata maoni yao kabla ya kupitisha sheria ambazo baadhi yake siyo rafiki na zinawaumiza.
Alitolea
mfano mabadiliko ya tozo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwaumiza.
Kwamadai kuwa wanaotengeneza kanuni na sheria hawajui matatizo na
vikwazo wanavyokutanavyo wafanyabiashara. Badala yake wamekuwa wakitoa maagizo tu.
Naye
Bakili Kilete anayefanyia biashara yake katika wilaya hiyo ya Kilwa,
alisema sheria zinazohusu misitu siyo rafiki kwa wafanyabiashara ikiwamo
na uwepo wa vizuizi vingi visivyo natija kwa serikali na
wafanyabiashara.
"Usumbufu
na wingi watozo unasababisha tutafute njia nyingine ili tupate faida,
maana kwa sheria zilizopo kama utataka utii na kutekeleza huwezi
kufanyabiashara hii," alisema Kilete.
Akijibu
malalamiko ya wafanyabiashara hao, mratibu wa usimamizi shirikishi wa
misitu nchini, Joseph Kigula, alisema sababu ya kuwepo vizuizi vingi ni
kwasababu baadhi ya wafanyabiashara sio waaminifu.
Akibainisha kuwa wafanyabiashara wangekuwa waaminifu kusingekuwa na sababu ya kuwa na vizuizi vingi.
Post a Comment