Shirika
la kimataifa la Amnesty limeitaka umoja wa kimataifa kuongeza nguvu kwa
wanajeshi wake wa kulinda amani katika Jamuhuri ya Afrika ya kati.
Vikundi
vya kutetea haki za binadamu vinasema kuna upungufu kwenye nguvu kazi na
vitendea kazi ambavyo vinapelekea raia kuwa katika hali ya hatari zaidi
katika mgogoro huo wa kivita.
Shirika
hilo linasema,jeshi la umoja wa mataifa limeshindwa kuzuia milipuko
iliyotokea katika mji mkuu wa Bangui mwezi septemba ambapo ulisababisha
watu zaidi ya ishirini na tano kuuwawa.
Afrika ya
kati ambayo imekuwa katika mgogoro tangu pale ambapo kikundi cha waasi
wa kiislamu wa Seleka kutoka madarakani mwaka 2013 ,na kuchochea ghasia
ya kulipiza kisasi kwa kikundi cha wapiganaji cha kikrosto.
Nchi hiyo
itarudia kufanya uchaguzi kwa kupiga kura ya kumchagua rais mpya ndani
ya wiki moja , na kampeni zinazotarajiwa kuanza siku ya Jumatatu.
|
Post a Comment