Mamilioni ya watu wenye asili ya China, duniani kote wanasheherekea mwaka mpya wa ki China .
Baruti
nyingi zilirushwa angani mjini Beijing ikiwa ni ishara ya kusheherekea
siku ya kwanza ya mwaka mpya wa nyani,Nyani wakiwa ni miongoni mwa
wanyama kumi na mbili wanaotumiwa kati ya alama za kichina katika
masuala ya utabiri.
Nako
mjini Yokohama nchini Japan, wao wanasheherekea siku kuu hii kwa
kuhesabu muda huku wakicheza ngoma ya asili ya kucheza na simba.
Maadhimisho
ya sherehe hizi za mwaka mpya zinajumuisha watu kula pamoja,kufanya
usafi na familia kuwa pamoja huku wakirusha fashi fashi angani.
|
Post a Comment