Mchezaji wa ziada Charlie Austin alifunga dakika saba baada ya kuingia na kuijeruhi Manchester United.
Manchester
United na meneja wao Louis Van Gaal walizomwa na mashabiki baada ya
timu hiyo kushindwa kufanya mashambulizi yoyote katika dakika 90.Wakati huohuo Adam Lallana alifunga bao la dakika za lala salama na kuiwezesha Liverpool kuishinda Norwich City 5-4 katika mechi iliojaa mashambulizi msimu huu.
Wes Hoolan alifunga bao la penalti kwa upande wa wenyeji kabla ya Jordan Henderson na Frimino kusawazisha.
James Milner aliiweka Liverpool kifua mbele huku Sabastian Basson akisawazisha lakini Lallana akafunga bao la Ushindi.
Post a Comment