![]() |
Watu 27
wamefariki na wengine kadha kujeruhiwa baada ya washambuliaji wa kujitoa
mhanga kujilipua katika kisiwa kilichoko katika Ziwa Chad.
Maafisa wa usalama nchini Chad wanasema washambuliaji walilenga soko ambalo hufunguliwa kila wiki katika kisiwa cha Loulou Fou.
Shambulio hilo limetokea chini ya mwezi mmoja baada ya serikali ya Chad kutangaza hali ya hatari katika eneo la ziwa Chad.
Hii
ilifanyika baada ya kuongezeka kwa mashambulio ya kigaidi kutoka kwa
wapiganaji wa Boko Haram kutoka nchini jirani ya Nigeria.
Chad
imekuwa ikisaidia Nigeria kukomboa maeneo mengi yaliyokuwa yametekwa na
wapiganaji hao wa Kiislamu ambao wameua maelfu ya raia.
|
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Post a Comment