Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee zenye maabara ya aina hiyo Afrika kusini mwa jangwa la Sahara
Tanzania ni moja
kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa
ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee kusini mwa Jangwa la Sahara zenye maabara ya aina hii ambayo itakuwa msaada mkubwa pia kwa nchi za jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR Dokta Mwele Malecela, amesema maabara hii ina umuhimu kwa kuwa itawezesha kufanyika kwa uchunguzi kwa urahisi na haraka zaidi, hata katika maeneo yaliyo na ugumu kufikiwa.
Post a Comment