0

 Boma la wajerumani lililopo wilayani Liwale mkoani Lindi likionekana baadhi ya kuta zake kuanguka chini
 Boma la wajerumani lililopo wilayani Liwale mkoani Lindi



 Boma la wajerumani lililopo wilayani Liwale mkoani Lindi hapa ni maeneo ya juu ya jengo hilo
 Mwandishi wa Liwale Blog Mwandae Mchungulike (wa upande wa kushoto) akiwa na wadau  alipotembelea kwenye jengo hilo hii leo
Baadhi ya milango ikionekana imefungwa kwa muda mrefu


 ndani ya chumba kwa juu jinsi lililopotengenezwa kwa uhodali


Picha zote na Liwale Blog
Boma la  wajerumani lililopo wilayani Liwale lililojengwa mwaka 1905  ukiachia lile ambalo lilichakazwa na moto kutokana na paa lake kuwa la majani linaendelea kupoteza uwezo wake na ingawa bado linatumika linastahili matengenezo makubwa ili kuwa baadaye moja ya kielelezo cha kuwapo kwa Wajerumani katika eneo hili la Liwale mkoani Lindi.

Liwale ingawa inakumbukwa sana kwa vita ya majimaji na jinsi wananhchi walivyoshiriki katika jaribio la kumuondoa mkoloni pia kuna maeneo ya matambiko ya Kingindo pia lipo kaburi na Mwanamama mmoja ambaye alikufa katika miaka ya karibuni ambapo wananchi mara nyingi hufika kulisafisha na kuomba baraka. Kaburi hilo lipo Ndapata.

Kwa mujibu wa historia huyo hakuwa mganga wa kienyeji lakini alikuwa na karama nyingi za kuzuia mabalaa na pia kuombea neema.

kwa mujibu wa  historia ya wazee walisema mama huyo hakuwa  uganga huyu ni kama vile ulivyouliza ni aina ya sharifu,alikuwa na karama za kama za mwanaume na hata viongozi wengi wakubwa walikuwa wanamtembelea kabla hajafa mwaka 1975”.

Walisema mama huyo alikuwa na nuwezo wa kuondoa janga la simba wanaposhambulia pia kuita mvua inapopotea au inapokuwa zaidi na kuifanya iwe ya kawaida.

Ikumkukwe kwamba Liwale ipo katika eneo la hifadhi ambapo Simba wakati mwingine huvamia makazi ya watu na watu walipoenda kumlilia mama huyu awasaidie samba hao walirejea porini wasionekane tena.

Kipaji cha pekee cha mwanamama huyo kinafanya bado hata umautini awavutie watu kwenda kulisafisha ziara lake kila wanapofika Liwale au kurejea Liwale. Na hata watu wengine wa Liwale kutoka maeneo yao hufika Ndapata kuzuru kaburi hilo na kulifanyia usafi.

Hali ilivyo sasa kama maeneo kadhaa yasipohifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo ipo hatari kubwa kwa vizazi vijavyo kukosa simulizi halisi la nini kilikuwapo au kutokea na kutegemea zaidi watu wa utafiti kutoka nje.

Sehemu kubwa ya mambo haya ya kihistoria yapo midomoni mwa watu wachache na kama tusipofanya juhudi za sasa kutafuta na kuhifadhi hatuwezi kuwa nayo baadaye, serikali ina wajibu mkubwa wa kuainisha vitu na kuanzisha makumbusho kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo wakati dunia ikiwa inabadilkika zaidi.


Hali ya boma ya mjerumani kwa sasa si nzuri lakini kama likitengenezwa au kukalabatiwa vyema kwa miaka kadhaa ijayo ikiwa ni moja ya alama ya kuwapo kwa watawala wa kigeni nchini.

Post a Comment

 
Top