0

Ujerumani imesisitiza kwamba ndiyo
inayowajibika kwa mauaji ya Wayahudi wakati
wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Hii ni baada ya Waziri Mkuu wa Israel
Benjamin Netanyahu kuibua mzozo mkubwa
baada yake kudai kiongozi mmoja wa
Wapalestina ndiye aliyewaambia viongozi wa
chama cha Nazi kuwaua Wayahudi barani
Ulaya.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel
alisema Wajerumani wanafahamu wazi
kwamba viongozi wa Nazi ndio waliopanga
na kutekeleza mauaji hayo yajulikanayo kama
Holocaust.
Netanyahu alikuwa amedai kiongozi wa Nazi
Adolf Hitler alitaka tu kuwafurusha Wayahudi
kutoka Ulaya, lakini Mufti Mkuu wa Jerusalem
Haj Amin al-Husseini akamwambia:
"Wachome moto."
Matamashi hayo yamekashifiwa vikali na
wanahistoria wa Israel pamoja na wanasiasa.
Akiongea kando ya Merkel mjini Berlin, Bw
Netanyahu alikuwa awali amesema "hakuna
anayefaa kukana kwamba Hitler aliwajibika
kwa kutekeleza mauaji ya Wayahudi".
Lakini Jumanne katika hotuba ya Baraza Kuu
la Wazayuni Duniani mjini Jerusalem, Bw
Netanyahu alidai Husseini ndiye aliyetoa wazo
la kuwaangamiza Wayahudi.
"Hitler hakutaka kuwaangamiza Wayahudi
wakati huo – alitaka tu kuwafurusha,”
aliambia kongamano hilo.
"Na Haj Amin al-Husseini alimwendea Hitler
na kusema: 'Ukuwafurusha, wote watakuja
hapa.’
“’Basi nifanye nini nao?’ [Hitler] alimwuliza.
Yeye [Husseini] akamjibu: ‘Wachome moto.'"

Post a Comment

 
Top