0

Mwaniaji wa urais nchini Marekani bi Hillary
Clinton anatarajiwa kutoa ushahidi wake mbele
ya wabunge wa Congress leo.
Kamati ya bunge inafanya uchunguzi kuhusu
shambulio kwenye ubalozi wa Marekani mjini
Benghazi nchini Libya lililofanyika miaka
mitatu ilopita.
Balozi wa Marekani nchini Libya na watu
wengine watatu waliuawa katika shambulio
hilo.
Bi Clinton alikuwa waziri wa maswala ya
kigeni.
Clinton sasa ni mpinzani mkuu kwenye
kinyanganyiro cha tiketi ya urais kwa chama
cha Demcratic.
Chama chake kimetaja uchunguzi huo kama
mbinu ya chama cha republican ya
kumchafulia jina.
Chama chake cha Democratic kinasema kuwa
uchunguzi huu wa sasa ni njama ya
wapinzani wao wa Republicans kumtupia
udongo na kunyima nafasi ya kuwa rais.
Tayari makamu wa rais Joe Biden amejiondoa
katika kinyang'anyiro hicho.
Biden alikuwa anatarajiwa kuttoa ushindani
mkali kwa bi Clinton.

Post a Comment

 
Top