0


1. Ukifika kituo chako cha kupigia kura panga
mstari, isipokuwa walemavu, wazee,
wajawazito na wanaonyonyesha wao
watapewa kipaumbele.
2. Mkabidhi msimamizi wa kituo kadi yako ya
kupigia kura ili
aihakiki.
3. Msimamizi wa kituo atasoma jina lako kwa
sauti ili Mawakala wote wa vyama vya siasa
wasikie, wakiwa na shaka
wakuhoji.
4. Pokea karatasi tatu za kupigia kura,
endapo wagombea wote
wanashiriki.
5. Nenda kwenye chumba cha kupigia kura
ambako kuna faragha na
utulivu.
6. Kwa kila nafasi, weka alama ya vema kwa
mgombea
unayemtaka na usiweke alama nyingine
yoyote maana kura yako itaharibika.
7. Kunja na utumbukize kila karatasi kwenye
sanduku husika;
urais, ubunge na udiwani.
8. Chovya kidole kidogo cha mwisho cha
kushoto kwenye wino
maalum kisha wapishe wengine nao wapige
kura yao
SHARE na wengine wajue

Post a Comment

 
Top