0

Shirika la Umoja wa Ulaya
linalopambana na maswala ya
uhamiaji haramu na biashara ya
binadamu, Frontex limetoa wito
kwa nchi wanachama wa umoja
huo kutoa msaada zaidi kwa nchi
tatu zilizoathirika kutokana na
kuwa na idadi kubwa ya
wahamiaji.
Ugiriki, Italia na Hungary ni nchi
zinazoelezwa kuathiriwa zaidi.
Shirika hilo limetaja hali hiyo
kuwa ya dharula na kutoa wito wa
kuongezwa kwa maofisa na vifaa
zaidi ili kushughulikia tatizo hilo.
Frontex imesema mwezi uliopita
zaidi ya Watu 107,000 waliwasili
ulaya kwa njia za panya, ikiwa ni
mara tatu zaidi ya waliowasili
mwezi Julai mwaka jana.
Watu hao wengi wanaelezwa
kutoka nchini Syria,Afghanistan
na nchi za kusini mwa jangwa la
Sahara wakikimbia hali mbaya ya
usalama na umasikini

Post a Comment

 
Top