0

Mazingira, tusipoyatunza tunafanana na yule
aliyeketi kwenye tawi la mti kisha akaanza
kulikata tawi hilo. Hata alipoonywa kwamba
kitendo hicho kilikuwa hatari kwake, yeye
aling’ang’ania. Matokeo yake ni kuwa
alianguka na tawi hilo. Pamoja na hayo,
hakuishia hapo kwenye ujinga wake. Alimsihi
yule aliyemwonya kuwa amtabirie na siku yake
ya kufa. Lo. Ni muhimu tutunze mazingira,
kwani bila mazingira endelevu, maisha na
ubinadamu vitafikia ukomo mara moja. Kwa
nini watu wachome misitu ovyo? Kwa nini
katika nchi ambapo gesi imevumbuliwa kwa
kiasi kikubwa bado tuendelee kutumia kuni
kama chanzo cha nishati? Tubadilike.
Share this:

Post a Comment

 
Top