0

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Mdemu, amesema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imeunda kitengo maalum cha kutafsiri sheria kutoka katika lugha ya Kingereza na kwenda katika lugha ya Kiswahili lengo ni kuwapa uwezo wananchi kuzielewa.

Bw. Mdemu ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam kwenye kongamano lililowakutanisha wanasheria kutoka sehemu mbalimbali waliokuwa wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, sambamba na kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wanasheria kwenye kazi zao.

Amesema baadhi ya watu wanaovunja sheria kutokana na kutoelewa vizuri namna ya utendaji kazi wa sheria hizo zinavyotaka hivyo wanapokea mapendekezo ya watu mbalimbali ambao ni walengwa wa sheria hizo na kuzifanyia kazi kwa haraka kwa kuwa walengwa ni wengi.

Amesema wanashirikiana na Bunge katika kuhakikisha wanawafikia wananchi walio wengi na kutoa elimu ya kutosha kupitia viongozi hao na wale wa vijiji.

Amesema ni wajibu wa kila mtu anayehusika katika kusaidia jamii afanye kwa wakati ili kuepusha mgongano baina ya serikali na wanachi wake pamoja na kushauri kwa kuzingatia msingi wa sheria, hivyo ni wajibu kwa wahusika kuzingatia misingi ya sheria.

Post a Comment

 
Top