0

Jumla ya kaya 460 zenye huitaji mkubwa katika mkoani Kagera ambazo hazina mahala pa kuishi kwa sasa baada ya nyumba zao za makazi kubomolewa kabisa na tetemeko la ardhi lilitokea mkoani humo ambalo lilisababisha madhara makubwa ambayo ni pamoja na vifo  zimenufaika na msaada wa vifaa vya ujenzi uliotolewa na shirika la World Vision Tanzania unaolenga kuzinusuru.

Vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na shirika hilo ni pamoja na saruji ambapo kila kaya iliyolengwa imepata mgao wa mifuko mitano ya saruji na vyandaru,kaya zilizopata mgao ni zile zenye watu wasio na uwezo kabisa wa kurejesha kwenye hali ya kawaida nyumba zilizoharibiwa na tetemeko ambao ni pamoja na wazee,wajane na wenye magonjwa ya kudumu,msaada huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mwantum Dau kwa waathirika hao wameshukuru msaada ambao umetolewa na kueleza changamoto waliyonayo ya kurudisha miundombinu ya majengo yao iliyoharibiwa.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na shirika la World Vision kwa niaba ya serikali,Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mwantum Dau amezihimiza kaya hizo kutumia misaada hiyo kulingana na malengo yaliyokusudiwa,naye Mratibu wa Kitengo cha maafa cha shirika la World Vision,Prosper Mujungu ameeleza shirika hilo kwa sasa linawasiliana na wafadhili ili liweze kuwafikia wale wote ambao nyumba zao zilianguka kabisa.

Post a Comment

 
Top