Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda cha
ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho muekezaji amekifanya kuwa
Ghala nakukitelekeza na watu kuiba vifaa na kufanya uharibifu mkubwa
Kiwanda hicho kipo wilaya ya Rungwe Mkoani Lindi Waziri Mkuu yupo katika
ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Rungwe Mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya magari yalivyo haribika
ambayo yalikuwa yanamilikiwa nakiwanda cha kukamua ufuta ILULU kiwanda
hicho kipo wilani Nachingwea Mkoani lindi ambapo mwekezaji aliye
kichukua amebadili matumizi na kukifanya Ghala lakuhifadhia bidhaa
kushoto kwa waziri mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi.
Picha na Chris Mfinanga
Na. Mwandishi Wetu, Nachingwea
Kutotumika kwa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kula cha Ilulu kumesababisha waziri mkuu, Kassim Majaliwa amuite mmiliki wa kiwanda hicho kilichokuwa mali ya umma.
Majaliwa
ametoa agizo hilo jana mjini Nachingwea alipokwenda kiwandani hapo ili
kuona maendeleo ya kiwanda hicho baada ya kununuliwa muda mrefu.
Waziri
mkuu baada ya kutoridhishwa na hali aliyoiona, amelazimika kumuita
mmiliki huyo aende ofisini kwake tarehe 22 mwezi huu, saa nne asubuhi
akiwa nanyaraka halisi za ununuzi aliofanya kutoka serikalini.
Majaliwa
alisema serikali haiwezi kuwavumilia wawekazaji na wanunuzi wa mali ya
umma wanaoshindwa kuendeleza na wanaobadilisha matumizi yaliyokusudiwa
na serikali.
Alisema
kutokana na wanunuzi na wawekezaji wengi kwenye miradi na mali za umma
kushindwa kuiendeleza, kunahaja ya kufanya mapitio ya sheria ya
uwekezaji ili kuona kama sheria zinaendana na lengo la ubinafsishaji.
"Maghala
na viwanda kama hivi bora vingekuwa mikononi mwa halmashauri,ipo haja
ya kupitia sheria za uwekezaji ili tuone kulitakiwa kufanyike
nini,sheria inasemaje na wawekezaji walitakiwa wafanye nini," alisema Majaliwa.
Kiwanda
hicho kabla ya kubinafsishwa kilikuwa kinatengeza mafuta ya kula
yanayotokana na ufuta.Hata hivyo hakuna uzalishaji unaoendelea kiwandani
hapo, majengo yake yamezungukwa na pori kukiwa hakuna dalili zozote za
kiwanda hicho ambacho kinatajwa kilinunuliwa na marehemu Abass Gulamali,
kuendelea na uzalishaji.
Post a Comment