Uamuzi huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.
Mlalamikaji alikuwa wakidai kwamba wakati NHC inamtoa kwenye nyumba alikuwa ndani ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa Mkataba wa Ubia Ulikuwepo lakini kwa kuwa haukutekelezwa ipasavyo. Na wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya Utekelezaji wake.
Mawakili wa Mbowe Hotels Mhe. John Mallya na Mhe. Peter Kibatala (pichani ) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao.
Post a Comment