Mahakama kuu ya Kenya
imemuachilia kwa dhamana
mshukiwa mkuu wa uwindaji
haramu aliyekamatwa nchini
Tanzania.
Feisal Mohammed
Ali,aliyeorodheshwa katika nafasi
ya sita ya watuhumiwa wa
uwindaji haramu na biashara ya
kuuza pembe za ndovu
ameachiliwa kwa dhamana baada
ya mawakili wake kuomba
mahakama hiyo imruhusu apokee
matibabu .
Hata hivyo afisi ya kiongozi wa
mashtaka ya umma nchini humo
tayari imeonesha kutoridhishwa
kwake na uamuzi uliofikiwa na
hakimu Davis Karani katika
mahakama ya Mombasa.
Hii si mara ya kwanza kwa
mahakama za Kenya kumruhusu
mshukiwa huyo kuondoka.
Mwezi Machi,Feisal alipewa
dhamana na mahakama ya
Mombasa lakini afisi ya kiongozi
wa mashtaka ya umma ikakata
rufaa iliyokubaliwa na mahakama
ya juu.
Hapo jana hakimu Karani alimpa
Feisal dhamana ya shilingi
millioni kumi za Kenya sawa na
dola laki moja $100,000 za
mMarekani
Feisal anakabiliwa na shtaka la
usafirishaji kinyume cha sheria
kwa tani mbili za pembe za ndovu
yenye thamani ya dola milioni
$4.5 za Marekani, umiliki wa
pembe za ndovu kinyume cha
sheria.
Yamkini Feisal anatuhumiwa
kuwa mmiliki wa pembe za ndovu
114.
Upande wa mashtaka unadai
kuwa yeye ndiye kiunganishi kati
ya wawindaji haramu
wanaolaumiwa kwa kuuwa tembo
33,000 kati ya mwaka wa
2010-2012 barani Afrika.
Feisal amekanusha mashtaka yote
dhidi yake.
Kasha la pembe hizo za ndovu
zilikuwa zimefichwa katika bohari
moja ya wauzaji magari mjini
Mombasa.
Punde baada ya polisi kuvamia
eneo hilo Feisal alitorokea
Tanzania alikokamatwa na polisi
wa huko baada ya ombi kutolewa
kupitia mtandao wa polisi wa
kimataifa Interpol.
imemuachilia kwa dhamana
mshukiwa mkuu wa uwindaji
haramu aliyekamatwa nchini
Tanzania.
Feisal Mohammed
Ali,aliyeorodheshwa katika nafasi
ya sita ya watuhumiwa wa
uwindaji haramu na biashara ya
kuuza pembe za ndovu
ameachiliwa kwa dhamana baada
ya mawakili wake kuomba
mahakama hiyo imruhusu apokee
matibabu .
Hata hivyo afisi ya kiongozi wa
mashtaka ya umma nchini humo
tayari imeonesha kutoridhishwa
kwake na uamuzi uliofikiwa na
hakimu Davis Karani katika
mahakama ya Mombasa.
Hii si mara ya kwanza kwa
mahakama za Kenya kumruhusu
mshukiwa huyo kuondoka.
Mwezi Machi,Feisal alipewa
dhamana na mahakama ya
Mombasa lakini afisi ya kiongozi
wa mashtaka ya umma ikakata
rufaa iliyokubaliwa na mahakama
ya juu.
Hapo jana hakimu Karani alimpa
Feisal dhamana ya shilingi
millioni kumi za Kenya sawa na
dola laki moja $100,000 za
mMarekani
Feisal anakabiliwa na shtaka la
usafirishaji kinyume cha sheria
kwa tani mbili za pembe za ndovu
yenye thamani ya dola milioni
$4.5 za Marekani, umiliki wa
pembe za ndovu kinyume cha
sheria.
Yamkini Feisal anatuhumiwa
kuwa mmiliki wa pembe za ndovu
114.
Upande wa mashtaka unadai
kuwa yeye ndiye kiunganishi kati
ya wawindaji haramu
wanaolaumiwa kwa kuuwa tembo
33,000 kati ya mwaka wa
2010-2012 barani Afrika.
Feisal amekanusha mashtaka yote
dhidi yake.
Kasha la pembe hizo za ndovu
zilikuwa zimefichwa katika bohari
moja ya wauzaji magari mjini
Mombasa.
Punde baada ya polisi kuvamia
eneo hilo Feisal alitorokea
Tanzania alikokamatwa na polisi
wa huko baada ya ombi kutolewa
kupitia mtandao wa polisi wa
kimataifa Interpol.
Post a Comment