Walinzi wa pwani wa Utaliano
wanasema kuwa wanaongoza
shughuli za kuwaokoa wahamiaji
kama elfu-tatu hivi ambao
wametuma ishara ya kuwa
taabani kwenye mashua nje ya
pwani ya Libya. Mashua kadha
zinashiriki katika uokozi.
Bahari baina ya Libya na Utaliano,
ndio njia inayotumiwa kwa muda
mrefu, na wakimbizi kutoka Afrika
na Mashariki ya Kati, ili kuingia
Ulaya.
Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja
wa mataifa unasema kuwa bahari
ya Mediterranea ndio kivukio
maarufu.
Kufikia sasa takriban watu laki
moja wamewasili katika ufukwe
wa Italia .
Wengine zaidi ya laki moja u nusu
160,000 waliwasili Ugiriki.
Jarida moja la Norway
Aftenposten, limesema kuwa
manuari ya kijeshi ya taifa hilo
Siem Pilot, liko njiani kuwasaidia
wahamiaji hao walioko
mashakani.
Manuari hiyo iliwaokoa wahamiaji
320 mapema leo kabla ya
kurejeshwa tena huko huko
kushiriki operesheni hii ya kuoko
nafsi za watu wanaokisiwa kuwa
takriban 3,000.
wanasema kuwa wanaongoza
shughuli za kuwaokoa wahamiaji
kama elfu-tatu hivi ambao
wametuma ishara ya kuwa
taabani kwenye mashua nje ya
pwani ya Libya. Mashua kadha
zinashiriki katika uokozi.
Bahari baina ya Libya na Utaliano,
ndio njia inayotumiwa kwa muda
mrefu, na wakimbizi kutoka Afrika
na Mashariki ya Kati, ili kuingia
Ulaya.
Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja
wa mataifa unasema kuwa bahari
ya Mediterranea ndio kivukio
maarufu.
Kufikia sasa takriban watu laki
moja wamewasili katika ufukwe
wa Italia .
Wengine zaidi ya laki moja u nusu
160,000 waliwasili Ugiriki.
Jarida moja la Norway
Aftenposten, limesema kuwa
manuari ya kijeshi ya taifa hilo
Siem Pilot, liko njiani kuwasaidia
wahamiaji hao walioko
mashakani.
Manuari hiyo iliwaokoa wahamiaji
320 mapema leo kabla ya
kurejeshwa tena huko huko
kushiriki operesheni hii ya kuoko
nafsi za watu wanaokisiwa kuwa
takriban 3,000.
Post a Comment