Wakazi wa kitongoji duni cha Mathare katika
mji mkuu wa Kenya, Nairobi, sasa wanaweza
kupata maji safi ya kunywa na kwa matumizi
mengine.
Mpango unaoungwa mkono na serikali
umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya
Nairobi unaowawezesha watu wanaoishi
kwenye mitaa ya mabanda kununua maji kwa
kutumia kadi.
Vituo vya kuuza maji vimebuniwa kote katika
sehemu za mabanda ambapo wenyeji hutumia
kadi zilizo na pesa kununua maji safi na kwa
bei nafuu.
Wenyeji wa mitaa ya mabanda nchini Kenya
wamekuwa na tatizo la kupata maji safi
ambapo hulazimika kununua maji kwa bei
ghali kutoka kwa wauzaji au kutoka kwa
magenge ambayo hudhibiti na kuuza maji
hayo kwa kuyachuuza.
Mradi kama huo umefaulu katika baadhi ya
maeneo ya vijijini nchini Kenya, lakini hii ni
mara ya kwanza kuzinduliwa katika mji huo
mkuu.
Vituo hivyo vya kutoa huduma hiyo ya maji
vimefanikiwa kutokana na ushirikiano kati ya
serikali ya mitaa nchini Kenya na kampuni ya
maji ya Grundfos ya Denmark.
Kampuni ya kusimamia huduma ya
usambazaji maji, ina mikakati ya kuhakikisha
kuwa huduma hii walioianzisha itasambazwa
kote katika mji mkuu wa Nairobi na
kwengineko nchini humo.
Huku hilo likianzishwa wakaazi wa mitaa
kadhaa mjini Nairobi bado wanalalamikia
ukosefu wa maji.
Maji ya ATM nchini Kenya
Post a Comment