0

Karenzi Karake
Mkuu wa upelelezi nchini Rwanda,ambaye
alikuwa anasakwa nchini Hispania kwa makosa
ya uhalifu wa kivita,sasa amekamatwa mjini
London.
Kitengo cha habari cha BBC cha BBC
Newsnight, kimegundua kwamba askari wa
kikosi cha Metropolitan walimkamata Karenzi
Karake kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow
mnamo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kikosi hicho cha askari wa Metropolitan tayari
kimethibitisha kwamba Karenzi ambaye sasa
ana umri wa miaka 54, amefikishwa katika
mahakama moja ya Westminster baada ya
kuwekwa kizuizini kwa hati ya kukamtwa ya
umoja wa ulaya, na atasalia kizuizini mpaka
mwishoni mwa wiki hii.
Karake alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa
usalama wa taifa wa Rwanda .Karake
alipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini Rwanda mwaka 1990 hadi mwaka 1994
na baadaye alipata cheo cha kamanda
msaidizi wa vikosi vya kulinda Amani vya
umoja wa mataifa huko Darfur. Karake ni
miongoni mwa makamanda walioko kwenye
orodha ya makamanda wa Kinyarwanda
wapatao 40 ,waliomo katika hati ya
mashitaka iliyotolewa mwaka 2008 na kikosi
cha uchunguzi cha Hispania kinachoongozwa
na jaji Andreu Merelles.
Mahakama hiyo ya nchini Hispania
inamtuhumu Karake, kwamba wakati
alipokuwa kiongozi mkuu wa kijeshi wakati
wa mauaji ya kimbari, aliamuru mauaji ya
watu kadhaa. Lakini pia kiongozi huyo wa
kijeshi anatuhumiwa pia kwa kuamuru mauaji
ya raia watatu wa Hispania waliokuwa
wakifanya kazi katika asasi moja ijulikanayo
kama Medicos del Mundo nchini Rwanda.
Kukamatwa kwa Karake kuna uwezekano
mkubwa wa kuiingiza serikali ya Uingereza
katika mgogoro wa kidiplomasia na nchi ya
Rwanda.
Inaarifiwa kwamba Mnamo mwaka 2013
Rwanda ilikuwa inashika namba 18 miongoni
mwa nchi zinazopokea misaada ya kiwango
cha hali ya juu kutoka Uingereza.
Karake ni wa kwanza kukamatwa miongoni
mwa makamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la
RPF kwa mashtaka yanayomkabili nje ya nchi
yake. Wakili Jordi Palou-Loverdos,
anayewakilisha watu 9 ambao wameuawa
wenye asili ya Hispania ameiambia BBC,
"Tunaamini kwa haki ya marehemu
ninaowasimamia itatendeka na haraka
Karenzi Karake atapelekwa mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili na huko
atajitetea yeye mwenyewe.
Na tunaamini kwamba wanasiasa na wengine
wenye mvuto na kesi yake hawataingilia kati
na kuizorotesha kesi, haki,ukweli na fidia
vitapatikana."

Karenzi karake

Post a Comment

 
Top