0
mwandishi wa Afrika kusini aporwa akijiandaa
kwenda hewani mbele ya kamera
Mwandishi maarufu wa runinga kutoka Afrika
Kusini ameibiwa hadharani alipokuwa
akijiandaa kwenda hewani mbele ya kamera.
Kanda ya video imewaonyesha wanaume
wawili wakimvamia Vuyo Mvoko, kutoka
yuninga ya taifa ya SABC ambaye alikuwa nje
ya hospitali moja ya mjini Johannesburg
akiripoti kuwasili kwa rais wa Zambia ili
kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.
Bwana Mvoko baadaye alisema kuwa mmoja
wa wezi hao alimtishia na bunduki alipokataa
kumpa simu yake ya rununu.
Wezi hao walionekana kutojali kamera
zilizokuwa mbele yao.
''Sikuelewa ni kwa nini waliweza kunivamia
mbele ya Kamera ilihali taa zote zilikuwa
zikiwaka na kamera zilikuwa zikinasa kila kitu
na, waliona kilichokuwa kikiendelea''.
Baada ya mda mfupi bwana Mvoko ambaye ni
mhariri wa kituo hicho cha habari alituma
ujumbe katika mtandao wake wa Twitter
akisema kuwa yuko salama salmin na kutuma
kanda ya video hiyo mtandaoni.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wezi hao
waliiba laptopu, na simu na kwamba maafisa
walikuwa tayari wanachunguza kisa hicho.
''Tunatumaini kwamba waliotekeleza kitendo
hicho watatambulika na kukamatwa'',

Post a Comment

 
Top