0
UPANDE wa utetezi katika kesi ya jinai
inayomkabili kiongozi wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Ponda
Issa Ponda umewasilisha hoja
zitakazoifanya Mahakama kutoona
sababu kwa mshitakiwa huyo kuwa na
kesi ya kujitetea.
Mawasilisho hayo yalifanywa mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
Mkoa wa Morogoro, Mary Moyo kwa zaidi
ya saa tatu na mawakili Juma Nassoro
na Abubakar Salim, wanaomtetea Ponda.
Akitoa mawasilisho hayo, Wakili Nasoro
alidai kuwa ushahidi uliotolewa na
upande wa mashtaka pamoja na vielelezo
vilivyotolewa mahakamani hapo, unatia
shaka na una udhaifu mkubwa,
unaomfanya mshtakiwa akose kesi ya
kujibu.
Alidai pia hati ya mashtaka yenye
makosa matatu, inaonekana kuwa na
mapungufu hasa katika shtaka la kwanza,
kwani imeshindwa kueleza ni kwa namna
gani mshtakiwa huyo alikiuka amri ya
Mahakama, kama alivyoshitakiwa katika
hati hiyo.
Alidai kuwa licha ya kushtakiwa kwa kosa
la kutotii amri halali ya Mahakama,
iliyotokana na hukumu, upande wa
mashtaka ulishindwa kuwasilisha hukumu
hiyo kama sehemu ya ushahidi.
Wakili huyo alidai kuwa hukumu
iliyotolewa Mahakama ya Kisutu dhidi ya
Ponda, haina amri yoyote inayoonesha
kuwa imetengeneza kosa kwa Shehe
Ponda, bali inaweza kuwa ni kukiuka
masharti, ambayo sio kosa la jinai.
Baada ya mawasilisho hayo, upande wa
mashtaka uliiomba muda Mahakama
kujibu hoja zilizokuwemo kwenye
mawasilisho hayo.
Mahakama iliridhia ombi hilo na
kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 20,
mwaka huu na hivyo mshtakiwa
kurudishwa rumande chini ya ulinzi mkali
wa poliai

Post a Comment

 
Top