0
Mama Maria Nyerere asema yuko hai
''Niko salama na buheri wa afya''
Hayo ni maneno ya Mama Maria
Nyerere ,mjane wa rais wa kwanza wa taifa la
Tanzania Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere,alipojitokeza na kupinga uvumi
ilokuwa ukienea kwamba ameaga dunia.
Madai kwamba Mama Maria alikuwa
amefariki yalisambazwa katika mitandao ya
kijamii siku ya jumatatu na kuzua wasiwasi
katika taifa la Tanzania kabla ya kujitokeza
na kukana madai hayo usiku katika runinga
ya taifa.
Akizungumza na vyombo vya habari
nyumbani kwake Masasani mjini Daresalaam,
kwa zaidi ya saa moja ili kuonyesha kwamba
yuko salama,amesema aligundua habari hizo
kupitia mkaza mwanawe ambaye alimpigia
simu
Alisema kuwa alipokea simu nyingi nyengine
kutoka kwa familia ambao waliuliza kuhusu
afya yake.
''lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa na
ushupavu wa kuniambia kuhusu uvumi wa kifo
changu ambao ulikuwa ukienea katika
mitandao ya kijamii.
''Kila mmoja aliyenipigia simu kabla ya
mwanangu alisema kwamba alitaka
kunisalimia'', alielezea akiongezea kwamba
hakuwa na wasiwasi kwa kuwa yeye ni mcha
mungu.
''Kwa kuwa mimi husali na kumuamini
mungu,sikushangazwa na habari hiyo kwa
kuwa hiyo ni kazi ya shetani ambaye
ameshindwa'',alisema.

Post a Comment

 
Top