Buriani Sylvester Marsh, utakumbukwa daima kwa mchango wako katika soka ya Tanzania
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA
kocha Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
Sylvester Marsh amefariki dunia Alfajiri ya leo katika hospitali ya
Muhimbili alikokuwa amelazwa.Taarifa
zinasema Marsh alikuwa amekuja Muhimbili kuhudhuria kliniki yake ya
kawaida juu ya maradhi ya saratani ya koo yanayomsumbua na ghafla hali
yake ikabadilika juzi hadi kufariki dunia.
Marsh
alianza kuwa Kocha Msaidizi wa timu za vijana Tanzania mwaka 2003 chini
ya Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ kabla ya mwaka 2006
kupandishwa timu ya wakubwa, akianza kumsaidia Mbrazil, Marcio Maximo na
baadaye Wadenmark, Jan Poulsen na Kim Poulsen.
Hata
hivyo, baada ya Jamal Malinzi kushinda Urais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) Oktoba mwaka juzi, alibadilisha benchi zima la ufundi la
Taifa Stars na Marsh akaondoka pamoja na Kim Poulsen. Sasa Mholanzi,
Mart Nooij ndiye kocha Stars, anasaidiwa na Salum Mayanga
Tangu
hapo Marsh amerudi kufanya kazi katika kituo chake cha Marsh Academy
mjini Mwanza, lakini mwaka jana ndipo maradhi ya saratani koo
yalipoibuka na akaletwa Muhimbili kwa matibabu.
Mfanyabiashara
Abdulfatah Salim, mmiliki wa hoteli ya Sapphire Court, alimsaidia kocha
huyo hadi akafanyiwa upasuaji na hali yake kuimarika Februari mwaka
jana na kurejea Mwanza.
Marsh
alipata ahueni ya kutosha na kuanza tena kazi ya kufundisha watoto wake
wa Marsh Academy, kabla ya wiki hii kuletwa Dar es Salaam kuhudhuria
kliniki.
Mbali
na timu za taifa, Marsh pia amefundisha klabu za Toto Africans ya
Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba na Azam FC ya Dar es Salaam.
Post a Comment